Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mbeya Ndugu Stella Kategile akitoa taarifa ya UKIMWI kwa mkoa wa Mbeya kwa ujumla wake. |
Dawa pamoja na vifaa tiba vilivyo nunuliwa kutoka katika fedha zilizo changishwa na wadau kwa ajili ya Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani. |
Na
Mwandishi wetu,Mbeya
Siku
chache mara baada ya Serikali kutangaza kuahirisha shughuli za
maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani ambayo yalipangwa kufanyika Kitaifa
mkoani Singida mwaka huu na badala yake pesa hizo zikatumike kununua Vifaa tiba
pamoja na Dawa za ARV hatimaye agizo hilo limetekelezwa na uongozi wa Mkoa wa
Mbeya .
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbasi kandoro, amesema
pesa zilizokusanywa na kamati ya inayoratibu maadhimisho hayo kwa mkoa wa mbeya
ni kiasi cha shilingi milioni 3.5 ambazo
zimetumika kwa ajili ya kutekeleza agizo hilo la rais Magufuli kwa ununuzi wa
ununuzi wa vifaa tiba pamoja na dawa hizo za ARV.
Amesema, kiasi hicho cha fedha kilipatikana
baada ya wahisani mbalimbali kuchangia na kwamba kiongozi huyo amewataka wadau
ambao hawakupata fursa ya kuchangia waendelee kwani mahitaji bado ni makubwa
hususani katika suala nzima la chakula.
Aidha, Mkuu huyo alitoa shukrani za pekee kwa
kanisa la Anglikan mkoa wa Mbeya kwa kuchangia boksi saba za kondomu na
kuwataka wananchi kuendelea kujikinga na maambukizi mapya ya virusi vya ugonjwa
wa ukimwi kwani hali ya takwimu bado si nzuri kwa Mkoa wa Mbeya.
Akizungumzia hali ya ugonjwa wa ukimwi kimkoa,
Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa, Stella Kategile, alisema kuwa kwa mujibu
wa matokeo ya utafiti wa kitaifa hali ya maambuki kwa VVU na UKIMWI uliofanyika
mwaka 2011/2012 unaonyesha Mkoa wa Mbeya unamaambukizi asilimia 9.0 ambayo ni
juu ya wastani wa kitaifa wa asilimia 5.1.
Hata hivyo, Kategille alitoa wito kwa
wananchi kushirikiana kwa hali na mali katika kutokomeza ugonjwa huo wa
UKIMWI kwenye jamii na hatimaye kutimiza kauli mbiu ya “Tanzania bila ya
Maambukizi mapya ya VVU, vifo vitokanavyo na ukimwi pamoja na unyanyapaa dhidi
ya wagonjwa inawezekana.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment