Tangazo
December 1, 2015
Tigo yafikisha upatikanaji wa huduma ya 4G LTE Dodoma
Mkuregenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) katika uzinduzi wa huduma ya 4G LTE jijini Dodoma, kushoto ni Meneja wa huduma ya 4G LTE, Benedict Mponzi
M
kurugenzi wa kanda ya Kaskazini kutoka Tigo Bw.George Lugata akimkabidhi Bw.Danson Kaijage kushoto laini mpya ya 4G LTE katika uzinduzi wa huduma ya 4G LTE, katikati ni Territory Meneja wa Dodoma,Singida na Kondoa Bw.Innocent Anthony kutoka Tigo jijini Dodoma.
·
Ni baada ya kuanza kutoa huduma hiyo kwa ufanisi jijini Dar es Salaam
Dodoma, Novemba 30 2015.
Wateja wa Tigo waishio Dodoma sasa wanaweza kupata mtandao wa intaneti wenye kasi kubwa zaidi kufuatia upanuzi wa upatikanaji wa huduma ya 4G LTE hadi kufikia jiji hilo lilopo kaskazini mwa Tanzania Teknolojia ya 4G LTE ina kasi mara tano zaidi kuliko teknolojia ya 3G inayopatikana nchini kwa sasa.
‘’Upanuzi huu umetokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika majaribio ya awali ya utoaji huduma ya 4G jijini Dar es Salaam kuanzia mapema mwaka huu’’, amesema Mkurugenzi wa kanda ya Kaskazini, George Lugata.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dodoma, Lugata amesema: "ni kielelezo cha jinsi ambavyo Tigo imedhamiria kufanikisha kuleta mabadiliko ya dijitali katika maisha ya watanzania na pia kuwa katika msitari wa mbele wa kutumia teknolojia ya kisasa na kibunifu nchini Tanzania."
Mtandao wa 4G LTE una kasi kubwa zaidi katika kuperuzi na kupakua kwa ahisi kutoka kwenye mtandao wa intaneti na pia katika kufanya mawasiliano kwa njia ya Skype. Huduma hii pia inaharakisha urushwaji wa picha za video na ubora hali ya juu na kufanya mikutano kwa njia ya mtandao.
“Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu waishio Dodoma kwamba sasa wanaweza kufurahia huduma bora zaidi za mawasiliano kutoka Tigo na Intaneti yenye kasi zaidi,” Lugata amesema. Dodoma ni moja wapo ya miji mikubwa Tanzania, na pia inajivunia Bunge la Tanzania na kwa sababu ya kuwa na vyuo viwili vikubwa Tanzania.
Wateja wote wa Tigo 4G LTE watanufaika na promosheni; kila atakapo ongeza salió la shilingi elfu moja au zaidi, atapata mb 500 bure kama bonasÃ.
A
metaja miji mingine katika mikoa sita ambapo 4G itaanza kupatikana hivi karibuni kuwa ni, Morogoro, Moshi, Mwanza na Arusha,Tanga na hapa Dodoma “jambo ambalo linaifanya Tigo kuwa na mtandao mkubwa wa 4G nchini Tanzania.” Lengo kuu ni kufikisha huduma ya 4G katika kila kona za nchi ifikapo mwaka ujao, Lugata ameongeza kusema.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment