Waziri Mkuu staafu Mizengo Pinda
akimkabidhi mguu mbadala Niyo Jonasi Mkazi wa Dar es Salaam ikiwa ni moja kati
ya miguu mbadala (bandia) 60 iliyotolewa bure na kampuni ya Kamal Group ya
Jijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kamal,
Sameer Gupta, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Reginald Mengi, Katibu
Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donald Mbando na Mwenyekiti wa Kamal
Group, Bwana Gagan Gupta. Picha na Mpigapicha wetu
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dar es Salaam,
Kampuni ya Kamal Group ya Jijini Dar es Salaam imetoa
miguu bandia yenye thamani ya mamia ya mamilioni ya shilingi kwa watu sitini
wenye ulemavu wa viungo na kuwafanya washerehekee Krisimasi wakiwa na uwezo wa
kutembea tena.
Kampuni hiyo pia imetoa vifaa vya kusaidia kusikia 40
kwa watu wenye usikivu hafifu.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo kwa
wahusika, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Bwana Satyam
Gupta alisema kampuni yake inaamini kuwa inao wajibu wa kusaidia maendeleo ya
jamii inayoizunguka.
“Tunaamini kuwa ni
wajibu wetu kusaidia jamii inayotuzunguka….ni wajibu wetu kuleta tabasamu
katika nyuso za watu wanaotuzunguka na kuhakikisha kuwa wale wenye ulemavu wa
miguu wanaweza kutembea tena,” alisema Bwana Satyam Gupta.
Naye mwenyekiti na
mkurugenzi mtendaji wa Kamal Group – kampuniinayojishughulisha na uzalishaji wa
nondo zinazokidhi viwango vya kimataifa - Bwana Gagan Gupta alisema
kampuni yake amefanikisha zowezi la utengenezaji miguu bandia kwa kutumia
wataalam kutoka India.
Wataalamu hao
waliletwa nchini ili waweze kutengeneza miguu hiyo hapa hapa nchini kwa kutumia
mitambo ya kiwanda cha Kamal kinachotumika kutengenezea nondo.
“Nia yetu ni
kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanarudi katika sehemu zao za kazi ili
watoe michango yao katika kuijenga Tanzania. Kwa vile tunacho kiwanda chenye
zana za kimataifa hapa hapa nchini Tanzania, tulilazimika kuwaleta wataalam tu
ili kazi yote waifanyie hapa hapa nchini. Tulichoagiza hapa kutoka nje ya nchi
ni malighafi tu,” alisema Bwana Gupta.
Wataalam hao ni
madktari kutoka katika taasisi yaBharat Vikas Parishad Viklang Kendra PaldiI, ya nchini
India ambao waliongozwa na Bwana Upendra Jani. Huduma kama hii itawafikia pia
watu wenye mahitaji kama hayo wanaoishi Arusha na Mwanza.
Naye mwenyekiti kitaifa wa Chama Cha Walemavu Tanzania
(Chawata) Bwana John Paul Mlabu alisema bei ya mguu mmoja bandia kwa sasa
inafikia Shilingi milioni nne na hivyo kuwafanya watu wengi washindwe kumudu.
Hii inamaanisha kuwa thamani ya miguu bandia 60 ni sawa na Shilingi milioni
240.
“Na ndio maana tunaishukuru sana kampuni ya Kamal kwa
msaada huu na tunaomba makampuni mengine nayo yawaige,” alisema.
Alisema Tanzania inakadiriwa kuwa na watu milioni
mbili wenye uhitaji wa viungo bandia ila kutokana na gharama kuwa kubwa, ni
asilimia 20 tu ndio wenye uwezo wa kumudu kuvipata viungo hivyo.
Katika
kuhudumia jamii, kampuni ya Kamal pia inaendesha mradi ujulikanao kwa jina Food
for Children (Chakula kwa watoto) ambapo kampuni hutoa chakula kwa
wanafunzi1,250 kila siku kwa shule za msingi za Nzasa ya Ilala na Kerege ya
Bagamoyo. Mradi huo ulioanza mwaka jana utarajia kuwafikia wanafunzi 3000 mwaka
2017.
No comments:
Post a Comment