Tangazo

December 9, 2015

TPB YASAFISHA SOKO LA FERI, YATOA VIFAA VYA USAFI, NI KATIKA KUUNGA MKONO UAMUZI WA RAIS MAGUFULI WA UHURU NI KAZI



Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Henry Bwogi, akizibua chemba ya kupitisha maji taka kwenye zoni 3 ya soko la samaki la kimataifa Feri jijini Dar es Salaam Desemba 9, 2015. TPB imeungana na watanzania katika kuunga mkono agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwataka wananchi kusherehekea sikukuu ya Uhuru wa Tanganyika kwa kufanya usafi ili kutekeleza zana ya “Uhuru ni Kazi” badala ya kufanya sherehe na matamasha huku nchi ikakabiliwa na ugonjwa wa Kipindupindu



Na K-Vis Media/Khalfan Said)

KATIKA kuunga mkono maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa wananchi na taasisi za serikali kufanya usafi siku ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanganyika, Benki ya Posta Tanzania, TPB, nayo iliungana na wananchi hususan eneo la soko la kimataifa la samaki Feri, katika kutekeleza agizo hilo.

Wakati Mh. Rais alishirikiana na majirani zake, wavuvi na wachuuzi wa samaki pale nje kidogo ya uzio wa Ikulu, hali ilikuwa hivyo hivyo kwenye maeneo mengi, ya nchi ambapo katika eneo hilo la soko la Feri, TPB walipewa eneo la kufanyia usafi kwenye zoni namba 1 na eneo la kuegeshea mitumbwi maarufu kama “Lebanon” ambapo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bw. Henri Bwogi, aliwaongoza wafanyakazi wa benki hiyo katika kufagia, kuzibua mitaro na chemba za maji taka, hali kadhalika kupakia taka kwenye malori ya kubebea taka.

Katika hatua nyingine Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bw. Bwogi, alikabidhi vifaa vya kufanyia uasafi viliovyokuwa vikitumiwa na wafanyakazi wa benki hiyo kwa uongozi wa soko ili waendelee na kazi ya usafi siku za usoni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, aliagiza sherehe za mwaka huu za Uhuru wa Tanganyika, zisherehekewe kwa kufanya kazi ili kutekeleza zana ya “Uhuru ni Kazi” badala ya kufanya matamasha na shamra shamra kwenye viwanja mbaklimbali nchini.

“ Nimefurahishwa sana na wananchi jinsi walivyojitokeza kwa wingi kwenye maeneo mbaklimbali ya nchi katika kufanya usafi ili kuiweka nchi yetu safi na kujikinga na maradhi kama Kipindupindu.” Rais Magufukli aliwaambia majirani zake baada ya zoezi la kufanya usafi.

Naye Kaimu Afisa Myendaji Mkuu wa TPB, Bw. Bwogi, alisema TPB kama taasisi ya serikali iliamuru wafanyakazi wake, wafike kazini na kushiriki katika kufanya usafi na sisi tumeona tuje kuungana na wenzetu wa feri ili kutekeleza maelekezo ya Rais wetu.” Alisema.


 Mfanyakazi wa TPB, akizibua chemba katika kutekeleza zana ya Uhuru ni Kazi

No comments: