Msimamizi wa kipindi cha Tv cha promosheni
ya Airtel mkwanjika Abdalah Wambua (kulia) akiongea mteja wa Airtel mara baada
ya namba yake kuibuka kuwa mshindi katika droo ya wiki ya tatu ya Airtel Mkwanjika
iliyochezeshwa katika ofisi za Airtel Makao makuu morocco jijini Dar es
salaam, chini ya usimamizi wa mwakilishi wa bodi ya michezo ya
kubahatisha Bwana Bakari Maggid (kushoto). Katika ni Afisa Masoko
ya Airtel bi Rebecca Mauma
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
.Washindi
28 kutoka katika mikoa mbalimbali wapatikana
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo
imechezesha droo ya wiki ya tatu ya promosheni ya Airtel Mkwanjika
na kuwapata washindi 28 ambao kila mmoja atapata nafasi ya kuingia kwenye
sanduku la pesa la Airtel na kujikusanyia pesa taslimu hadi kiasi cha shilingi
milioni moja Promosheni ya Airtel Mkwanjika imekuwa ni promosheni ya kipekee inayowapatia
wateja wanne wa Airtel kila siku kuchagulia kupitia droo inayoendeshwa chini ya
usimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nafasi ya kuingia kwenye
kisanduku kinachopeperusha pesa na kupewa dakika moja ya kujikusanyia pesa kasha kuondoka
na mkwanja wao wa pesa taslimu.
Akiongea na waandishi wa habari, Afisa Uhusuiano
wa Airtel bi Jane Matinde alisema , "mpaka sasa tunao washindi 72 kutoka
katika mikoa mbalimbali nchini kati yao wahsindi 44 wameshajishindia
kiasi cha pesa walichoweza kujikusanyia ndani ya sanduku la pesa,
hivyo tunajisikia furaha kuwawezesha watanzania na
wateje wetu kwa ujumla kuboresha maisha yao kwa kuwapatia kiasi cha pesa kama
zawadi ya ushindi wao kupitia promosheni hii ya Airtel Mkwanjika .
Washindi 28 tuliowapata leo nao pia watapata
nafasi ya kuingia kwenye kisanduchu cha pesa na kujizolea mkwanja hadi kiasi
cha shilingi milioni moja.
Akiwataja washindi hao Matinde alisema
washindi wa droo ya wiki ya tatu ni pamoja na Issa Salim Kiame kutoka
mkoa wa Pwani, Joseph Malingo kutoka Zanzibar, Amina Yusufu mkazi, Hamisi
Chande, Ashraf Jumanne, Edwin Mtei, Abdallah Mahambi, Simon Seleman, Abdallah
Hamis, Saleh Mohmaed, Derick Shirima, Salumu Mgwela na
Juma Mnende kutoka mkoa wa Dar es salaam wengine ni Erastus Mutachuba na
Justine Muganyizi kutoka Bukoba, Manyama Masata kutoka Sengerema Mwanza, George
Christian, Mfumbi Vicent, Antony Mluge, Junior Haji kutoka mkoa wa Morogoro,
Jessi Mlei mkazi wa Arusha, Bahati Muhawala mkazi wa mkoa wa Mbeya Pamoja na Annastazia Myengwa kutoka
mkoa wa Mara.
Matinde
aliongeza kwa kusema , kila mteja wa Airtel ana nafasi ya kujishindia, ni
rahisi mteja anachotakiwa kufanya ni kununua vocha yake, kukwangu
na kuingiza kwenye simu yake au kununua muda wa maongezi kupitia Airtel Money
au kununua vifurushi vya Airtel yatosha na namba yake itaingizwa moja kwamoja itaingia
kwenye draw ya promosheni ya Airtel Mkwanjika.
"Natoa wito kwa watanzania na wateja wetu
nchi nzima kuendelea kutumia huduma zetu na kuongeza salio ili kupata nafasi ya
kuibuka kuwa washindi kupitia promosheni hii ya Airtel Mkwanjika"
alisisitiza Matinde
No comments:
Post a Comment