Tangazo

March 14, 2016

Airtel FURSA yaingia Dodoma yatoa msaada wa milioni 9/-

Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (katikati), akijaribisha moja ya mashine mashine walizomkabidhi kijana Fikiri Chinji (kushoto), anayejishughulisha na ufundi seremala, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye karakana yake iliyojengwa na Airtel katika Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa Dodoma mwishoni mwa wiki hii. Anayeshuhudia (kulia) ni Meneja mauzo manispaa ya Dododma Hendrick Bruno.
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa pili kulia), akimkabidhi kijana Fikiri Chinji (wa pili kushoto), anayejishughulisha na ufundi seremala, msaada wa vifaa mbali mbali vya ufundi na kujengewa karakana mpya kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye karakana yake iliyojengwa na Airtel katika Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa Dodoma mwishoni mwa wiki hii. Wanaoshuhudia ni Wazazi wa Fikiri John Chinji baba, (kushoto) na mama mzazi Erika. 
Wanakijiji wa Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa Dodoma wakiangalia banda alilokabidhiwa  Kijana Fikiri Chinji (hayupo pichani) anayejishughulisha na ufundi seremala, pamoja na msaada wa vifaa mbali mbali vya ufundi kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, mwishoni mwa wiki hii.

 XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
· Airtel FURSA kusaidia kikundi cha wajasiliamali 30 Dodoma

Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA umeendelea na utekelezaji wa  ahadi yake ya kuwawezesha wajasiliamali wawili kila wiki nchini kwa kutoa misaada yenye thamani ya hadi shilingi milioni 10 kwa kikundi au kijana atakaeotoa mchanganuo na kusimamia biashara itakayoweza kusaidia kuongezea kipato na kupunguza umasikini katika jamii .

Wiki hii Airtel FURSA imeingia mkoani Dodoma na kukabidhi vitendea kazi vyenye dhamani ya shilingi milioni 9 kwa  kijana mjasiliamali Fikiri Chinji anaeishi katika kijiji cha Ng”ong”ona ili aweze kuendeleza shughuli zake za useremala na kuweza kuajiri vijana wengine wanaomzunguka.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano katika kijiji cha Ng”ong”ona Dodoma  Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Dangio Kaniki alisema “vifaa alivyoomba ndio tunavyomkabidhi ni pamoja na mashine yakupiga msasa, mashine kwaajili ya kutobolea na kutengeneza urembo pamoja na nyingine yakuranda mbao. Pia tumejenga kalakana yake hapa kijijini ili apate mazingira mazuri ya kufanyia kazi zake kwa ustadi  na kufundisha vijana wengine kujiajiri kupitia mradi huu”

“Airtel Fursa tumeona ni muhimu kumuwezesha kijana huyu  aweze pia kuongeza thamani ya vitu anavyotengeneza na  kuviuza kwa bei nzuri, vile vile tumejipanga kuja tena Dodoma hivi karibuni na tutasaidia kikundi cha ujasiliamali kiitwacho PAMBANA cha Dodoma Mjini chenye jumla ya vijana 30 ambapo wasichana ni 20 na wavulana 10 na kinajishughulisha na usafi wa mazingira na kutengeneza sabuni” alieleza Dangio
  
Akipokea Vifaa hivyo huku akishangiliwa na wanakijiji wenzake, kijana Fikiri  ameishukuru Airtel fursa kwa kuona umuhimu wa  kumpiga jeki kwa kumwezesha vifaa na sehemu ya kufanyia shughuli zake,

“Sasa nitafanya kazi zangu kwa ufanisi mkubwa ikiwa ni pamoja na kutengeneza bidhaa zitakazokubalika sokoni, naishukuru sana Airtel Fursa kwa kunishika mkono” Alisema Fikiri


Mradi wa Airtel FURSA uko katika msimu wa pili ambapo tokea kuanzishwa kwake umefanikiwa kuandaa na kufanya semina za ujasiliamali 17 na kukutana na vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24 zaidi ya 3000, pia hadi sasa imeweza kutoa misaada kwa vijana na makundi ya vijana  hao wajasiliamali zaidi ya  108 kwa lengo kuwaongezea uzalishaji na kipato.

No comments: