Tangazo

March 14, 2016

DUKA KUBWA LA KAMERA ZA KISASA LA DEO FILIKUNJOMBE LAZINDULIWA DAR

 Mkurugenzi wa Mauzo wa Kampuni ya Jumbo Camera House, Mathias Luoga akionesha vifaa mbalimbali vya kamera wakati wa uzinduzi wa duka jipya lililopo Jengo la NSSF Benjamin Mkapa, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Sara Filikunjombe,  mke wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ludewa, marehemu Deo Filikunjombe ambaye pia mmiliki wa kampuni hiyo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA: KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mke wa marehemu Filikunjombe, Sara  (wa pili kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Prodaction, Ritta Poulsen (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Jumbo Camera House, Paul Buckendahl (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Mauzo wa Kampuni hiyo, Mathias Luoga wakigongeana glasi zenye Champagn wakati wa hafla hiyo.
 Wageni waalikwa wakioneshwa moja ya kamera na vifaa vyake inayouzwa katika duka hilo kubwa la aina yake kwa Afrika Mashariki, Kati na Kusini.

 Paul akiwaongoza wageni waalikwa kusimama kwa dakika moja kumkumbuka marehemu Deo Filikunjombe
 Mgeni rasimi katika hafla hiyo, Ritta Poulsen akihutubia wakati wa uzinduzi wa duka hilo

 Kamera ya kisasa ya kupigia matukio kwa juu
 Baadhi ya wageni waalikwa
Mkurugenzi wa Kampuni ya Jumbo Camera House, Sara Filikunjombe akiwa na Ritta na mmoja wa wageni wakati wa hafla hiyo.
 Baadhi ya vifaa vya kamera
 Wageni walikwa wakiangalia vifaa mbalimbali vya kamera dukani humo
 Sasa ni wakati wa furaha

No comments: