Tangazo

March 1, 2016

TPB YATOA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA SACCOS KIGOMA, NI MPANGO WA KUINUA MITAJI YA WAJASIRIAMALI


Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya, (kushoto), akimpatia mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 75 Kaimu mwenyekiti wa Saccos ya Ishimwe Kigoma Bi.Gabriela Hangula wakati wa hafla ya kukabidhi fedha kwa vikudi vya benki za vijijini (VICOBA), mkoani humo,. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma. John Ndungulu, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Tanzania, (NEEC), Bi. Beng’ Issa na Afisa Mtendaji Mkuu, (CEO) wa Benki ya Posta Tanzania, Bw. Sabasaba Moshingi.Benki ya Posta imekabidhi jumla ya silingi milioni 175 kwa vikundi hivyo viwili ikiwa ni mpango wa kuwawezesha wananchi kwa kuwakooesha fedha kuinua mitaji yao chini ya udhamini wa baraza hilo.


Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya (kushoto), akimpa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100 Mwenyekiti wa Saccos ya TWCC Kigoma, Dorothy Takwa. Wa pili kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma John Ndungulu, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Uchumi Tanzania Bi. Beng’ Issa na Afisa Mtendaji wa Benki ya Posta Sabasaba Moshingi akishuhudia makabidhiano hayo.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Sabasaba Moshingi akiongea na wana-saccos wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji, kabla ya kuwakabidhi kiasi cha fedha Shs milioni 175/=kama mkopo ili kuinua mitaji yao. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, John Ndungulu, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Tanzania, (NEEC), Bi. Beng’ Issa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya.



Mkurugenzi wa Idara ya Mikopo wa Benki ya Posta Tanzania, Henry Bwogi akimpa zawadi mmoja wa mwanachama wa Saccos, kulia ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Benki Tanzania, Timotheo Mwakifulefule.


No comments: