Tangazo

February 28, 2016

FULL MKANDA PAMBANO LA CHEKA NA MSERBIA LEADERS JANA, CHEKA ASHINDA KWA ...'.POINTI'

 Bondia Mtanzania Francis Cheka (kulia) akichapana na mpinzani wake bondia kutoka nchini Serbia, Geard Ajetovic, wakati wa pambano lao la raundi 12 la ubingwa wa Mabara , uzito wa Super Midle wa WBF lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Katika raundi ya kwanza bondia Cheka alionekana kuanza kwa woga na kumfanya mpinzani wake kumshambilia kwa ngumi za kushitukiza na kumpeleka chini, jambo lililomfanya Cheka kuchanganyikiwa na kuhesabiwa na mwamuzi na kisha kuendelea na pambano.

Baada ya kwenda chini katika raundi ya kwanza raundi ya pili cheka alionekana kucheza kwa tahadhari kubwa kwa kupiga na kukimbia huku mpinzani wake akionekana kujigadi muda wote na kupiga ngumi za kushitukiza zilizokuwa na madhara kwa Cheka.
Katika pambano hilo Bondia Francs Cheka, aliibuka na ushindi kwa pointi
 Cheka akijitahidi kupangua konde la mpinzani wake....
 Cheka, alichanika katika raundi ya nane baada ya mpinzani wake kumbananisha kwenye kona iliyokuwa na utelezi ambapo aliteleza na kupoteza mwelekeo na kushambuliwa mfululizo. Na Mafoto Blog.
KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
 Cheka akijibu mapigo....
 pambano likiendelea....
 Wakiliana taimingi.....
 Mimi sijui hapa Cheka alikuwa akifanya kitu gani sijui alikuwa akikwepa konde ama akijihami kwa kutoka nduki....
 Muda wote Mserbia alionekana kujihami kwa staili hii.....
 Cheka akitupiamo ......
 Hapa sasa hata mimi sijui ilikuwa ni kitu gani kwamba ni konde zito, mieleka ama nini.....
 Cheka sijui alikuwa akifanya nini hapa....
 Mserbia akitupiamo....
 Mwamuzi akimhesabia Cheka baada ya kuanguka katika raundi ya kwanza.....
 Cheka akitangazwa mshindi kwa pointi na mwamuzi kutoka chama cha ngumi WBF....
 Cheka akishangilia ushindi wake.....
 Mashabiki wakimbeba cheka kwa furaha.......
 Cheka akivishwa mkanda wa ubingwa.....baada ya kutangazwa mshindi....
Mabondia wa kike, Lulu Kayage wa Dar es Salaam (kushoto) akichuana na mpinzani wake Mwanne Haji wa Mbeya, wakati wa pambano lao la utangulizi...Katika pambano hilo Mwanne aliibuka kidedea kwa pointi.
 Sehemu ya mashabiki waliohudhuria mapambano hayo wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea ulingoni...
 Mwanne (kulia) akimwadhibu Lulu....
 Sehemu ya wanahabari waliokuwepo kuripoti pambano hilo....
 Mabondia Mohamed Matumla (kushoto) na Bakari Mohamed, wakipambana katika moja ya pambano la utangulizi...katika pambano hilo,Matumla alishinda kwa pointi.
 Cosmas Cheka (kulia) akichapana na Mustapha Dotto katika pambano lao la utangulizi, Katika pambano hilo, Cosmas alishinda kwa pointi.
 Mwenyekiti wa Club ya Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' akimvisha mkanda wa ubingwa wa WBF Cosas Cheka baada ya kumchapa mpinzani wake kwa pointi.
 Cosmas akipiga picha na mapromota wake baada ya kutangazwa mshindi...
 Dullah Mbabe wa Dar es Salaam (kulia) akichapana na Bakari Mwakansope, Katika pambano hili Dullah mbabe, alishinda kwa K/O katika raundi ya Nne.
 Mawe yakiendelea.....
 Mawe......
 Wakiendelea kuchapana....
 Mwakansope akipelekwa chini kwa konde zito......
 Mwakansope akipata maelekezo kutoka kwa msimamizi wake, Karama Nyilawila........
 Pamoja na maelekezo kibao lakini aliporudi tu ulingoni alikutana na konde zito lililompeleka chini kama hivi....
Mwamuzi akimhesabia Mwakansope...

No comments: