Tangazo

April 18, 2016

Airtel yazindua Duka la kwanza katika Wilaya ya Kahama

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Vita Kawawa akikata utepe kuzindua duka jipya la kisasa la Airtel wilayani humo mkoani Shinyanga jana, litakalowawezesha wananchi kupata huduma bora za mawasiliano. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Lyamba  na  (kushoto) ni Meneja Mauzo wa Mkoa wa Shinyanga, Ezekieli Nungwi. PICHA: HISANI YA AIRTEL
XXXXXXXXX
Kampuni ya simu za Mononi ya Airtel  Tanzania  imeendelea na mikakati yake ya kusogeza huduma bora kwa wateja wake kwa kufungua duka lake la kwanza katika wilaya ya kahama  Shinyanga

Duka hilo la kisasa ni moja ya ahadi ya Airtel kujali wateja wake Tanzania nzima na kuwapa huduma iliyobora na ya kiwango cha juu popote pale walipo.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Mkurugenzi  wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel, Adriana Lyamba alisema, “ Airtel  imefanikiwa  kuwafikia wateja kwa kufungua milango mjini Kahama na kuwahakikishia tunaendelea kuwa wabunifu  kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora za kisasa zenye gharama nafuu kwa watumiaji wa simu za mkononi nchi

Duka hili ni la kwanza hapa mjini kahama, hivyo tunajisikia furaha sana kuleta huduma zetu karibu na wateja wetu na kuwapatia fursa ya kutumia huduma zetu kama vile Airtel Money kujiongezea kipato. Natoa wito kwa wakazi wa Kahama kupata nafasi ya kutembelea duka hili na kupata huduma pamoja na bidhaa mbalimbali ikiwemo modemu ya maajabu ya Airtel Wingle pamoja na simu orijino za smartphone kwa bei nafuu. Aliongeza Lyamba

 Kwa upande wake Mgeni rasmi katika uzinduzi huo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Vita Kawawa alisema “Kahama ni  moja ya miji inayokuwa kwa kasi kubwa hivyo kufunguliwa kwa duka hilo  kutaongeza ufanisi wa huduma za mitandano. 

Tunawashukuru sana Airtel kwa kuona ni vyema kutuletea huduma hii hapa mkoani na kutuhakikishia mawasiliano bora wakati wote na kuondoa changamoto zilizoko hapo awali. Kwa wakazi wa kahama huu ni wakati muafaka kutumia duka hili vyema ili kupata bidhaa zitakazotusaidia katika kuendesha shughuli zetu za uchumi na kijamii

  Mpango huu wa Airtel kufungua  maduka  zaidi nchini, unalenga kuboresha maduka ya kampuni hiyo, ili yawe ya kisasa kama ilivyo katika mikoa ya  mwanza, Arusha,Kilimanjaro na Mlimani City  Dar es
Salaam.

No comments: