Na Mwandishi Wetu
WAREMBO 14 wamejitokeza kushiriki katika shindano la kumsaka
malkia wa Tabata mwaka huu ‘Miss Tabata 2016’.
Mratibu wa shindano hilo
Joseph Kapinga alisema jana kuwa warembo hao wanaendelea na mazoezi kila siku
kwenye Ukumbi wa Da West Park, ulioko Tabata jijini Dar es Salaam.
Aliwataja warembo hao
kuwa ni pamoja na Latifa Dibwe (18), Salma Abeid (18), Fatma Mapunda (19),
Dinnah David (22) na Joyce Kweka (24).
Wengine ni Neema Makwaia
(22), Jesca Daniel (22), Sabrina Kipunga (22) Happiness Mnyeke (20), Grace
Matiko (20), Olanda Filima (19),Neema Zablon (21),Joyce Nyimbo (24) na Noela
Kyombya (24).
Naye Mkurugenzi wa
shindano hilo ambaye pia ni mkuu wa kambi, Godfrey Kalinga alisema kuwa warembo
hao wanafundishwa na Neema Mchaki ambaye alikuwa ni mkufunzi wa shindano la
Miss Ilala na Miss Tanzania 2014.
Kalinga aliwaomba
warembo wengine wenye sifa kujitokeza kushiriki kwenye shindano hilo ambalo
huvutia wadau wengi wa sanaa ya urembo nchini.
“Bado tunapokea warembo,
tunataka kufanya shindano la kihistoria mwaka huu na tumepanga kuwapeleka
washiriki kwenye mbuga za wanyama ili kupromoti utalii wa ndani,” alisema Kalinga.
Aliongeza kuwa washiriki
watano watakaoshika nafasi za juu katika shindano hili wataiwakilisha Miss
Tabata kwenye shindano la Kanda ya Ilala ‘Miss Ilala’ na baadaye Miss Tanzania.
Miss Tabata inaandaliwa
na Keen Arts ambayo ni kampuni tanzu ya Bob Entertainment wakati Ambasia Mallya
ndiye mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata.
Alizitaja kampuni
zilizothibitisha kudhamini Miss Tabata kuwa ni CXC Africa, Fredito
Entertainment, Saluti5 na Bob Entertainment.
No comments:
Post a Comment