Mmoja ya majaji
wa shindano la Airtel Trace Music Stars ambaye ni mtangazaji wa TV mahiri,
Mwanamuzi, Mwigizaji na mfanya biashara, Jokate Urban Mwegelo (wa kwanza
kulia) akiongea na jopo la majaji wenzake wakati wakichagua vijana waliofudhu
kuingia kumi bora katika wiki hii. Zoezi hili lilifanyika katika ofisi za makao
makuu ya Airtel Tanzania zilizoko Moroco jijini Dar es Saalam.
Xxxxxxxxxxxxxxx
DAR ES SALAAM
Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel Leo imetangaza washiriki kumi bora wa wiki wa shindano kubwa
barani Afika lijulikanallo Airtel Trace Music Stars lililolizinduliwa mwanzoni
mwa mwezi wa pili na kuwapatia fursa vijana kuonyesha vipaji vyao.
Kabla ya kutangaza washindi hao Jopo la majaji linaloshirikisha
wasanii na wataalamu wa muziki akiwemo mtangazaji wa TV mahiri, Mwanamuzi,
Mwigizaji na msanii aliyejikita katika maeneo mengi, Jokate Urban
Mwegelo, mtunzi wa nyimbo na mwaimu wa Muziki Anthony Joseph Namata“JOETT
pamoja na mtengenezaji wa Muziki na mfanyabiashara Luciano Gadie Tsere
likikaa mwishoni mwa wiki na kuchagua waimbaji 10 bora kati
ya vijana walioweza kushiriki mpaka sasa.
Akitangaza baadhi ya vijana waliioingia katika kumi
bora , Jaji Anthony Joseph Namata“JOETT alisema “moja kati ya vigezo
vilivyotumika kuwapata hawa walioingia kumi bora ni pamoja na uwezo wao wa
kuimba pamoja na sauti lakini pia idadi ya kura anazozipata kutoka
kwa wasikilizaji.
Hivyo basi napenda kuchukua fulsa hii kutangaza vijana
waliofanikiwa kuingia katika kumi bora ambao ni pamoja na Teddy Benedict Code 55210241, Beny Sule
Code 55210243, Eddy Zone (Jack) Code 55210245, Anneth Stanley Code
55210248, Sarah Code 55210249, Nicole Grey Code 55210253, Yvone Masai Code
55210254, Adili Kwezi Code 55210115, Anneth Komba Code552101256 , David Benson Mahenge Code 55210244”.
Kwa
upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema “Tunafurahi
kuona vijana wengi wamejitokeza kushiriki na kuonyesha vipaji vyao kwa mwaka
huu, natoa wito kwa vijana kuendelea kushiriki kwani mashindano bado
yanaendelea.
Sambamba
na hilo tunawaomba watanzania wawapigie kura washiriki wanaowapenda pamoja na
vijana hawa ili waweze kuendelea kutetea nafasi zao na hatimae kuingia kwenye
tano bora na kisha kupenya kwenye fainali za kitaifa zitakazofanyika hapa
jijini Dar es saalam mwishoni mwa mwezi Mei”.
‘Ili kupiga kura kwa mshiriki unaempenda unatakiwa kupiga 0901002233 Kisha kuingiza code namba ya mshiriki
au tuma SMS yenye code ya namba ya mshiriki kwenda namba 15594” aliongeza
Mmbando.
Huu ni msimu wa pili wa Shindano la Airtel Trace Music Stars
ambapo sasa shindano hili lipo katika hatua kitaifa, fainali za taifa
zinategemea kufanyika 20 Mei 2016 ambapo mshindi wa kwanza atajishindia shilingi
million 50, pamoja na kupata nafasi ya kwenda kushiriki katika mashindano ya
taifa mwezi Juni Lagos nchini Nigeria. Mshindi wa pili ataondoka na
shilingi million 5 na watatu shilingi milioni 2.
Ili kushiriki piga namba 0901002233.rekodi
wimbo wako sasa.
No comments:
Post a Comment