Tangazo

October 19, 2016

DOLA 20,000 KUCHUKULIWA NA WABUNIFU WA KIDIGITALI KATIKA TUZO YA TANO YA MWAKA YA TIGO KIDIGITALI YA CHANGE MAKERS

Meneja wa Huduma za kijamii wa Tigo Woinde Shisael akizngumza na wanahabari wakati wa Uzindizi wa shindano hilo leo Jijini Dar es salaam 
 Kampuni ya simu ya Tigo kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Reach For change wamezindua shindano la Tuzo ya mwaka ya kidigitali ya Tigo Change Makers, shindano linalolenga kuwatambua na kuwasaidia wajasiriamali jamii kwa kutumia zana za kidigitali na Technologia katika kuboresha Jamii pamoja na matokeo yake kwa Vizazi vya Baadae,ambapo kwa mwaka huu Tigo inaangalia ubunifu uliojikita katika mtazamo wa elimu kupanua kujumuisha kidigitali na ambao unalenga kusaidia shiughuli za Ujasiriamali.
 Faraja Nyarandu Pichani  alishinda dola 20,000/- Mwaka 2014 katika shindano la @TigoTanzania #DigitalChangemakers.leo akizungumza mafanikio aliyoyapata baada ya ushindi na kuwezeshwa na Tigo Tanzania
Jumla ya fedha taslim dola za marekani 20,000 zitatolewa kwa kila wazo litakaloshinda kati ya mawazo mawili yatakayoshinda na hivyo kutoa  nafasi ya kuingia katika malezi ya Reach For change,mafunzo ya kibiashara na mtandao wa dunia wa wajasiriamali wengine wa kijamii.ambapo kipindi cha kutuma maombi kwa ajili ya kushiriki katika shindano hilo kimefunguliwa Rasmi leo hadi November 21,2016.

Akiangumza katika mkutano wa wanahabari wakati wa uzinduzi huo Meneja wa Huduma za kijamii wa Tigo Woinde Shisael amesema kuwa Tigo inayo furaha kuendesha Tuzo ya kidigitali ya Tigo change makers mwaka huu ikiwa na mtazamo Mpya,huku akisema kuwa Timu ya tigo ina hamu sana ya kusaidia Ubunifu wa Kidigitali na shughuli za ujasiriamali nchini Tanzania.

Shisael ameongeza kuwa Tuzo ya kidigitali ya Tigo Changemakers ni niia kubwa ya kuwasaidia wabunifu kijamii wazuri walio na weledi ambao wanahitajika nchini katika kuwawezesha kubadilisha maisha ya jamii kupitia masuluhisho ya Kidigitali.
Ikiwa ni mwaka wa Tano ambapo Tigo Reach For change wanaendesha shindano hilo la kutafuta mjasiriamali jamii,Bi Woinde amepongeza kazi za washindi waliotangulia na kuhimiza wengine kushirikiana nao katika mawazo yao.
“Hivi sasa tutawasaidia wajasiriamali 9 kupitia mkakati wa kidigitali wa Tigo Changemakers.wametumia vizuri fedha walizopewa,mafunzo ushauri,na Zaidi ya yote kuleta mabadiliko nchini Tanzania”amesema Meneja huyo wa Huduma za kijamii Tigo.
Carolyne Ekyarisiima Mshindi wa mwaka 2015 akieleza machache mbele ya wanahabari
Akitaja mifano ya washindi ambao wamenufaika na shindano hilo tangu lianzishwe  amesema kuwa Carolyne Ekyarisiima ni mmoja washndi wa tuzo ya Tigo Change makers ambaye amekua akifanya kazi ya kuziba pengo la kijinsia katika Technologia ya Habari na mawasiliano kupitia ujasiriamali kijamii wa Vifaa na watoto wa kike(Apps &girls)
“Mwaka 2015 Carolyne alileta mabadiliko kwa wasichana 1000,kupitia mfumo wa klabu mashuleni, warsha,maonesho,mawasiliano ya simu,kambi za mijadala na mashindano”amesema Shisael na kuongeza kuwa “sio tu kwamba mkakati huu unasaidia kuhakikisha watoto wengi wa kike kuzifikia Teknolojia za kidigitali,hali kadhalika inawezesha kuwa Viongozi wa baadae wa Teknolijia Ya habari na mawasiliano.

Carolyne ni mmoja wa mfano wa wabunifu weledi wa kidigitali ambao Tigo inawatafuta ili iwasaidie kupitia tuzo ya mwaka huu,Shisael amesema anatarajia kupitia Upya ubunifu wa kidigitali wa kuvutia ambao utawasilishwa katika shindano la mwaka huu.

No comments: