Tangazo

November 22, 2016

KAMPUNI YA SIMU YA TIGO YATANGAZA OFA YA KRISMAS YA SMARTPHONE

 Ofisa Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya Simu ya Tigo,  Shavkat Berdiev (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kampuni hiyo kutangaza ofa ya Krismas ya Smartphone. Kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga.
 Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

Kampuni inayooongoza kwa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania  leo imetangaza  kuzindua ofa  mpya  ya Tecno Y3+ Music Smartphone  ambayo imejengewa ndani yake  zana kubwa  ya kuchezesha  ambayo inatoa nafasi ya kutiririsha  kupitia mtandao na hivyo kuwawezesha wateja kufurahia na kusherehekea na wapendwa wao wakati wa kipindi hiki cha kipekee  kinachohusiana na Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

Akitangaza ofa hiyo katika mkutano wa waandishi wa habrai jijini Dar es Salaam,  Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigom, Shavkat Berdiev alisema kuwa Simu ya mpya ya kisasa ya Smartphone  tayari ipo katika maduka yote ya Tigo na mawakala nchi nzima  na inapatikana kwa gharama ya shilingi 99,999 tu. Hii ni aina ya kwanza ya simu ya kisasa ya Techno Smartphone  kuingizwa katika soko  ikiwa na zana kubwa (Boom App) ilibeba miziki ya ndani.

“Tunaamini  ofa hii  itawawezesha wateja wengi wa Tigo  kufurahia manufaa ya simu hii ya kisasa inayouzwa kwa bei ya reja reja ambayo mteja anaimudu,  ikiwemo kupata mtandao wa intaneti  ambao uko pamoja na  kujikita kwetu katika  kuboresha mabadiliko katika maisha ya kidijitali,’ alisema Berdiev.

Aliongeza, “Hali kadhalika imekuwa ni utamaduni wetu  kuwapatia  wateja simu nzuri ya kisasa  wakati wa msimu wa sikukuu. Hivyo  natoa wito kwa wateja wetu  wote  hususani wale wanaosafiri  kwenda  mikoani  hadi maeneo ya vijijini  kuungana na familia zao kuchukulia faida  ya kuwepo kwa ofa hii.”

Akizungumza katika  tukio hilo Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga  aliongeza;Pindi mteja anaponunua simu, moja kwa moja Tigo  inamzawadia mteja huyo GB 1  ya data za intaneti na   muda wa maongezi shilling  5,000  Tigo kwenda Tigo kila mwezi kwa kipindi cha mwaka mmoja (miezi 12).


Simu ya Kisasa ya Y3+ imekuja  na vitu mahsusi vya kipekee ambavyo  vinajumuisha  betri iliyoboreshwa maisha,  sehemu mbili  za kadi za simu,  uwezo wa kuhifadhi data kwa kiwango cha GB 8  pamoja na kasi ya ufanisi  512 (RAM) ambazo zinaifanya kuendesha na kuhifadhi data.

No comments: