Tangazo

November 8, 2016

MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO, MHANDISI FELCHESMI MRAMBA, ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA KINYEREZI II

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (mbele kulia), akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa gesi wa Kinyerezi II jijini Dar es Salaam
NA K-VIS BLOG/KAHLFAN SAID

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (anayezungumza pichani), amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa umeme wa gesi wa Kinyerezi II utakaozalisha umeme wa Megawati 240 unaotekelezwa na shirika hilo jijini Dares Salaam.

Mradi huo ulizinduliwa Machi 2016 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, kuweka jiwe la msingi  ambapo eneo hilo lilikuwa pori tu kazi ya kusafisha eneo ili kuanza ujenzi ilianza mieziminane iliyopita.

“Kwa wale waliokuwepo siku Mheshimiwa Rais anaweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huu, mtakumbuka kuwa eneo lote hili lilikuwa pori, napenda niwapongeze wahandisina mafundiwote mnaotekeleza ujenzi huu kwa kazi nzuri nakasi ya kuridhisha.” Alipongeza Mhandisi Mramba, ambaye alitembelea eneo hilo mwishoni mwa wiki kukagua maendeleoyaujenzi wake.

Wahandisi wa TANESCO wakishirikiana na wenzao kutoka SUMITOMO CORPORATION NA TOSHIBA za Japan na washauri wa mradi Lahmeyer International ya Humburg nchini Ujerumani, ndio wanaojenga mitambo hiyo kwa ambapo unatekelezwa kwa fedha za walipa kodi wa Tanzania na Japan.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi huo, Meneja Mradi, Mhandisi Stephen Manda alisema ni pamoja na ujenzi wa msingi wa kitalu namba moja (Foundation Works Block I na ujenzi wa msingi watenki la kuhifadhia maji (raw water tank).

“Kazi inaendelea vizuri napenda kukujulisha kuwa baadhi ya vifaa muhimu vimekwisha wasili na tunachosubiri pengine kufikia mwezi Januari ni kuwasili kwa mashine zenyewe (Turbines), hivi sasa tuko kwenye mazungumzo na watu wa TANROAD na mamlaka nyingine kuhusu utaratibu wa kusafirisha mitambo hiyo kutoka bandarini kuiletahapa.” Alifafanua Mhandisi Manda.

Akielezea zaidi kuhusu manufaa ya mradi huo pindi utakapokamilika, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhanidis Felchesmi Mramba alisema, TANESCO iliwaahidi watanzania kuwa kwa kushirikiana na serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya umeme ikiwa ni pamoja na kuzalisha umeme mwingi zaidi ili hatimaye uende sambamba na malengo ya serikali yaawamu ya Tano ambayo imedhamiria kujenga nchi ya viwanda.

“Nia yan Mheshimiwa rais ya kujenga nchi ya viwanda itafanikiwa kwa vile sasa umeme mwingi na wa uhakika utapatikana ili kuhudumia viwanda vilivyopo na vipyavinavyoendelea kujengwa.”Alihitimisha Mhandisi Mramba.


 Mhandisi Mramba, (kulia), akiongozana na Meneja Mradi wa ujenzi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephen Manda
 Ujenzi wa msingi wa tenki la kuhifadhia maji (raw water tank)
 Ujenziwa msingi wa moja ya sakafu ya kufunga mashine za kufua umeme, (Foundation work block)

 Mhandisi Manda, (kulia), akifafanua masuala mbalimbali yahusuyo maendeleo ya ujenzi huo
 Mhandisi Manda akiwasilisha taarifa ya hatua mbalimbali za ujenzi wa mradi huo
 Jengo la muda la utawala
 Kazi ya kuhamisha kifusi ikiendelea
 Mhandisi Manda aakionyesha kitu
 Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshughulikia miradi ya usafirishaji na usambazaji umeme, Mhandisi Gregory Chegere (kulia), akizungumza jambo na mmoja wa Wahandisi viongozi kutoka kampuni ya TOSHIBA ya Japan
 "Mambo swafi" ndivyo anavyoonekana akisema, Mhandisi Mramba, wakati akianza ukaguzi wa mradi huo akifuatana na Meenja Mradi, Mhandisi Manda (kushoto)
 Mameneja na maafisa wa TANESCO waliofuatana na Mkurugenzi Mtendaji kutembelea eneo hilo
 Mhandisi kiongozi wa kampuni ya TOSHIBA
Mameneja na maafisa wa TANESCO

No comments: