Tangazo

December 19, 2016

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA WAFANYABIARA WA CHINA HAPA NCHINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Chama Cha Wafanyabiashara wa China nchini Tanzania ambao walimtembelea ofisini kwake leo.
                                       .............................................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini China kuja kuwekeza nchini katika maeneo mbalimbali ikiwemo uvuvi katika bahari,madini, utalii, ujenzi wa viwanda na miundombinu.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Watendaji Wakuu wa makampuni makubwa kutoka nchini China ambao walikuja hapa nchini kutafuta fursa za uwekezaji.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wawekezaji hao kuwa Tanzania ni nchi salama kwa ajili ya kuwekeza kutokana na amani iliyopo na kwa sasa Serikali inaendelea na mkakati kuondoa vikwanzo vinavyokwamisha uwekezaji ikiwemo ukiritimba na rushwa nchini.
Amesema Tanzania na China zinamahusiano mazuri na ya muda mrefu hivyo ni muhimu mahusiano hayo yakaendelea kuimarishwa zaidi kama hatua ya kukuza biashara kati ya nchi hizo mbili kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa Tanzania na China.
Amesisitiza muhimu wa kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya Chama cha Wafanya Biashara wenye Viwanda na Wakulima nchini (TCCIA) na  Chama cha Wafanya biashara kutoka China kama hatua ya kuimarisha kwa angalia fursa bora za uwekezaji kati ya China na Tanzania.
Makamu wa Rais pia ameishukuru nchi ya China kwa kuichangua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi Nne za bara la Afrika kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda.
Kwa upande wao, Watendaji hao wa makampuni makubwa kutoka nchini China wamesema kwa sasa wapo mbioni kujenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza vifaa tiba katika eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam na wameshapewa ekari 160 kwa ajili ya kujenga kiwanda hicho.
Watendaji hao wameiomba serikali ya Tanzania isaidie kuhakikisha pindi mradi huo utakapoanza kujengwa huduma za msingi ikiwemo umeme na maji zinapatikana kwa urahisi kwenye eneo hilo.

No comments: