Tangazo

December 23, 2016

MKUU WA WILAYA YA ILALA, SOPHIA MJEMA AKABIDHI ZAWADI ZA KAPU LA SIKUKUU JIJINI DAR

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (katikati), akimkabidhi zawadi, Asha Soud ambaye ni mshindi la shindano la Kapu la Sikukuu Dar es Salaam leo, lililoendeshwa na Kampuni ya Multichoice Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Redio cha EFM. Kutoka kulia ni msanii Haji Salum 'Mboto' Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Joseph na Mkurugenzi wa EFM, Francis Cizza.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (katikati), akimkabidhi zawadi msanii Irene Paul.
 Maelekezo ya upokeaji wa zawadi hizo yakitolewa.
 DC Mjema akizungumza na wanahabari baada ya kukabidhi zawadi hizo.
 Washindi wa shindano hilo wakiwa katika picha ya pamoja.
 Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Joseph (kulia) akimkabidhi zawadi Kelvin Mhenzi
Washindi wakiondoka na zawadi zao.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ametoa zawadi mbalimbali kwa washindi 24 wa shindano la Kapu la Sikuu lililoendeshwa na Kampuni ya Multichoice Tanzania na Kituo cha Redio cha EFM.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi hizo Dar es Salaam leo DC Mjema aliwataka wananchi kuendelea kufuatilia kwa karibu vipindi mbalimbali vinavyotangazwa na kituo hicho ili waweze kujipatia zawadi kutokana na kujibu maswali yatokanyo na vipindi hivyo  na kuweza kupata zawadi kama walizopata wenzao katika kipindi hiki cha Sikukuu.

"Napenda kuwapongezwa EFM kwa shindano hili kwani linatoa msukumo kwa wananchi wa kusikiliza vipindi mbalimbali vyenye manufaa" alisema Mjema.

Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Joseph akizungumza katika hafla hiyo alisema kampuni hiyo kupitia kisambuzi chake cha DSTV imemwaga zawadi ya visambuzi vya kisasa vipatavyo 24 pamoja na vifurushi vya mwezi mzima kwa washindi wa shindano hilo la Kapu la Sikuu.

"Washindi hao wataweza kusherehekea Sikukuu ya krismas na mwaka mpya kwa kuangalia chaneli zaidi ya 70 za DStv ikiwemo mpira wa ligi ya Hispania (Laliga) na ligi ya Uingereza" alisema Joseph

Alpha alisema Multichoice Tanzania haijawatunuku washindi hao 24 wa kapu la Sikuu pekee bali watanzania wote kwa ujumla kwani hivi karibuni walishusha bei za vifurushi vyao kwa wastani wa asilimia 16, huku kifurushi maarufu cha DStv Bomba chenye chaneli zaidi ya 70 kikipunguzwa bei hadi sh.19,975 tu.

Zawadi hizo kwa washindi hao zilitolewa na wasanii waigiza maarufu nchini kama Muhogo Mchungu, Riyama Ali, Haji Salum Mboto na Hashim Kambi wanaoonekana katika Tamthilia ya Huba.

No comments: