Tangazo

March 8, 2017

WAFANYAKAZI WANAWAKE WA PPF WAUNGANA NA WENZAO KUSHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI


Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakifurahia wakati wa kusherehekea siku ya Wanawake Duniani kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Machi 8, 2018.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

WAFANYAKAZI Wanawake wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, leo Machi 8, 2017, wameungana na wenzao katika kusherehekea siku ya Wanawake Duniani kwenye viwanja vya Mwembe- Yanga jijini Dar es Salaam.

Katika maadhimisho hayo yaliyohanikizwa na mvua za rasharasha, wanawake hao wakiwa na furaha, walipita mbele ya viongozi wakuu wa mkoa na kuonhyesha mabango yao yaliyokuwa na ujumbe tofauti tofauti.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mwaka huu yanaongozwa na  kauli mbiu isemayo “Tanzania ya viwanda, Wanawake ndio Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi”.
Kauli mbiu hiyo inalenga kuikumbusha jamii kuhusu umuhimu wa kujenga mazingira wezeshi kwa Wanawake  hasa kutambua mchango wao  katika kuleta Maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla.

Katika maadhimisho hayo ya siku ya Wanawake Duniani Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva, ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye awali Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ilisema Mkuu huyo wa Mkoa ndiye angekuwa mgeni rasmi lakini hakutokea.

Katika hotuba yake, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, alisema  jamii inapaswa kutimiza wajibu wake ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha, kuwaamini na kuwapa Wanawake haki sawa katika nafasi za Elimu, Uchumi na uongozi ili wawe chachu ya mabadiliko yenye lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

 Baadhi ya akina mama wa taasisi ya THTU nao wakipita mbele ya jukwa kuu.

No comments: