Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadala akizungumza wakati wa mafunzo elekezi
ya kuwajengea uwezo watendaji na viongozi wa Majimbo 9 ya CCM na jumuiya zake
Mkoa wa Mjini Unguja.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR
NAIBU
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Abdalla Juma Saadala "Mabodi"
amezitaka jumuiya za Chama hicho kutumia vizuri fursa ya uchaguzi kuwapitisha
viongozi wenye sifa na uwezo wa kukiletea ushindi chama katika Uchaguzi mkuu wa
mwaka 2020.
Kauli
hiyo ameitoa wakati akifungua mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo viongozi wa
majimbo Tisa (9) ya Chama na Jumuiya za Mkoa wa Mjini juu ya mabadiliko ya
Katiba ya CCM ya 1977 yaliyofanyika hivi karibuni yaliyofanyika Katika ukumbi
wa mkoa huo Aman Unguja.
Alisema uchaguzi unaofanyika hivi sasa katika kwa
ngazi mbali mbali za Chama hicho ndio uwanja wa kuandaa jeshi kamili la kisiasa
lililokamilika kila idara na lenye ujuzi na mafunzo yote ya vita ya kisiasa
litakaloweza kupambana kwa ujasiri na kufanikisha ushindi katika uchaguzi mbali
mbali za Dola ili CCM iendelee kushinda na kutawala kupitia utaratibu wa
Kidemokrasia.
Aliwasihi washiriki wa mafunzo hayo kutumia vyema
mafunzo hayo ya siku moja ili waweze kuwa na uelewa mpana wa Mabadiliko kadhaa
yaliyofanyika ndani ya katiba ya CCM ili watekeleze kwa ufanisi majukumu yao na
kuwaelimisha wanachama wengine juu ya taaluma hiyo.
Dkt.Mabodi alieleza kwamba matarajio ya taasisi hiyo ya
kisiasa ni kuona kasi ya mabadiliko ya kiutendaji kwa haraka hasa
kwa viongozi na watumishi wa Chama na jumuiya zake.
Pia aliongeza kwamba mbali na matarajio hayo mafunzo
hayo yatamaliza mizozo na malalamiko yaliyokuwa yalisababisha kutokuwepo kwa
ufanisi mzuri wa kiutendaji kwa baadhi ya maeneo ndani ya Mkoa huo.
Naibu Katibu Mkuu huyo alisema hatovumilia tabia za
kupangwa safu za viongozi kwani kufanya hivyo ni kukiuka Kanuni za
maadili na miongozo ya uchaguzi huo.
"Tumekuwa
tukisema siku zote kuwa CCM ndio mwalimu wa Demokrasia yaani hivyo vyama vya
upinzani demokrasia na ustaarabu wa kisiasa tumewafunza sisi hivyo dhana hizo
lazima tuzisimamie na kuzitekeleza kwa vitendo kupitia uchaguzi unaoendelea
ndani ya taasisi yetu.", alisema Dkt. Mabodi na kuzitaka kamati za
uchaguzi na maadili kufuatilia kwa kina mwenendo wa uchaguzi na watakapobaini
kasoro watoe taarifa kwa ngazi husika ili zitafutiwe ufumbuzi wa haraka.
Alifafanua kwamba kupitia uchaguzi huo panatakiwa
kupatikana viongozi na watendaji watakaoendeleza siasa za upendo, maendeleo,
umoja pamoja na mshikamano unaojali misingi ya kidemokrasia ndani na nje ya
taasisi hiyo.
Hata hivyo alieleza dhamira ya chama hicho kupitia
mabadiliko yaliyofanyika katika Katiba ya Taasisi hiyo kuwa ni pamoja na kila
mwanachama kujipanga kisaikolojia kusaidia kuimarisha uchumi wa CCM kupitia
rasilimali zilizopo sambamba na kubuni miradi mingine ya kimaendeleo.
Sambamba
na hayo kupitia Mafunzo hayo Dkt.Mabodi aliwakumbusha washiriki hao kwamba ili
wafanikiwe katika utendaji wao ni lazima watumie vizuri rasilimali watu ya
wazee wa CCM pamoja na wastaafu katika sekta za umma na binafsi kwani wana
uwezo na uzoefu mkubwa wa kushauri na kutoa maelekezo mazuri juu ya
masuala mbali mbali ya kiutendaji ndani ya Chama hicho.
Mapema
akizungumza katika mafunzo hayo Mwenyekiti wa Mkoa huo, Nd. Bora afya Juma
Silima alisema Mkoa huo umejipanga kufanikisha kwa ufanisi uchaguzi huo ili
kulinda historia ya chama hicho katika kufanikisha uchaguzi unaoheshimu misingi
ya utawala bora na demokrasia kwa wananchi wote.
No comments:
Post a Comment