Tangazo

May 17, 2017

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MAFUNZO YA SIKU TATU YA POLISI WANAWAKE KUTOKA SHIRIKISHO LA MAJESHI YA POLISI KUSINI MWA AFRIKA (SARPCO)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya siku tatu ya Polisi Wanawake kutoka Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCO) kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Muonekaniko wa picha kutoka juu ukionyesha Wajumbe wakati wakimsikiliza  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suuluhu Hassan kwenye ufunguzi wa Mafunzo ya siku tatu ya Polisi Wanawake kutoka Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCO) kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi Mkazi wa UN nchini, Alvaro Rodriguez akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya siku tatu ya Polisi Wanawake kutoka Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCO) ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
 Mwaziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya siku tatu ya Polisi Wanawake kutoka Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCO) kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suuluhu Hassan akizungumza na Askari wa Kike wa Kikosi cha Kuzuia Fujo (FFU) mara baada ya kufungua Mafunzo ya siku tatu ya Polisi Wanawake kutoka Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCO) kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
                        ..............................................................................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka askari polisi wanawake kutoka kwenye Shirikisho la Majeshi la Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) washiriki kikamilifu katika oparesheni mbalimbali ambazo zinafanyika kwenye ukanda huo kama hatua ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku Tatu ya Polisi wanawake kutoka nchi wanachama wa SARPCCO katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza askari polisi wanawake kufanya kazi kwa bidii na kujituma hatua ambayo itasaidia kupanda vyeo kama  askari wanaume katika maeneo yao ya kazi.

Amesisitiza kuwa muda wa kulalamika kuwa hawapandishwi vyeo umeshapitwa na wakati bali kwa sasa wachape kazi na waonyeshe kuwa wanaweza majukumu yao wanayopangiwa ili waweze kupanda vyeo.


“Vyeo haviji tu ni lazima polisi wanawake muonyeshe kuwa mnaweza ili muweze kupandishwa vyeo na kupata nafasi za uongozi katika Majeshi yenu

Kuhusu utendaji kazi wa Polisi wanawake, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka polisi hao kutumia mkutano huo wa siku Tatu kujadili kwa kina namna ya kuondoa changamoto hizo zinazorudisha nyuma utendaji wao wa kazi.


Amesema kama polisi wanawake wataacha majungu na kujenga umoja na mshikamano miongoni mwao watafikia malengo yao haraka hasa katika kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu ikiwemo biashara ya dawa za kulevya.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amesema anaimani kubwa kuwa mafunzo hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa polisi hao wanawake kuimarika ipasavyo katika utendaji wao wa kazi.

Masauni pia amewahimiza polisi wanawake wanaopata mafunzo hayo kwenda kuwaelimisha na wenzao mipango na mikakati waliyoweka katika kulinda raia na mali zao katika nchi zao.

No comments: