Na Jumia Travel Tanzania
Kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma za hoteli kwa njia ya mtandao ndani na nje ya bara la Afrika, Jumia Travel imedhamiria kukomboa jitihada za masuala ya usafiri kupitia kampeni yake mpya itakayojulikana kwa ‘DemocratizeTravel.’
“Dhumuni letu kubwa ni kuondoa mawazo yaliyojengeka miongoni mwetu haswa linapokuja suala la mchakato mzima kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Hii inamaanisha kupunguza gharama hususani za malazi, upatikanaji wa taarifa pamoja huduma bora kwa kila mtu. Pia kupitia kampeni hii tunataka kuwaonyesha wateja wetu uzuri uliofichika kuhusu bara la Afrika kwa kuwapatia suluhu ya mahitaji yao yote pindi wanapotaka kusafiri kama vile; hatua au mambo ya kuzingatia, malazi, chakula na shughuli za kufanya mahali waendapo,” alisema Bi. Dharsee.
“Hatutoishia hapo bali tunataka pia kuondoa mitazamo tofauti ya kwamba sehemu za kutembelea zilizopo nchi za Magharibi kama vile Ulaya na Marekani au Dubai ni bora zaidi ya Afrika.
Mbali na kuwarahisishia waafrika kusafiri kwenye maeneo waliyopo lakini pia tunawawezesha kuvuka mipaka kwenda sehemu zingine duniani. Hapa msafiri ataweza kulipia gharama za kusafiri, kwa mfano kwenda jijini London nchini Uingereza, kwa fedha ya nchi yake anayotokea. Hayo yote yanawezekana na yamerahishwa kwani kupitia mtandao wetu mteja ataweza kukata tiketi ya ndege na kufanya huduma ya malazi kwa sehemu anayokwenda kwa wakati mmoja,” aliongezea Meneja Mkaazi wa Jumia Travel nchini.
Kampuni hiyo imesema mbali na kuelekeza kampeni hiyo kwa wateja wake lakini pia itawashirikisha hoteli washirika katika kuhakikisha wanawafikia wateja na kukua kwa haraka zaidi.
Hayo wanayahakikisha kupitia kuwatangaza mtandaoni ili kukuza muonekana na biashara zao, kuwapatia mifumo ya teknolojia inayoendana na soko la Afrika ili kuwarahishia uendeshaji wa biashara zao kama vile Extranet, SMS au barua pepe pamoja na kuchochea utoaji na uboreshaji wa huduma bora ili kuwavutia wateja wengi zaidi.
“Uzinduzi wa kampeni hii utakwenda sambamba na uwasilishaji wa ripoti yetu ya masuala ya ukarimu na utalii barani Afrika ambayo tutaitoa siku chache zijazo. Kwenye ripoti hii tumezungumzia masuala yote tuliyoyaona kuhusiana na mustakabali mzima wa sekta hii kwa ujumla.
Lakini pia kutakuwa na shughuli zingine zinaendelea kwenye mitandao ya kijamii kama vile kwa wateja wetu kuwashirikisha wenzao picha au video fupi za sehemu walizotembelea, walijisikiaje na walivutiwa zaidi na vitu gani,” alihitimisha Bi. Dharsee.
No comments:
Post a Comment