Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw. Ronald Manongi, (katikati), akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko, Bw. Valence Luteganya, (kulia) na Meneja Masoko, Bi. Rahma Ngassa, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2017.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
MWALIMU
Commercial Bank PLC imezindua kampeni ya
“Weka Akiba na Ushinde” kwa Wateja wake na wananchi kwa ujumla.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2017 wakati akizindua kampeni hiyo, Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw. Ronald Manongi alisema, “Draw
hiyo ipo wazi kwa wateja wote waliopo na watakaojiunga na sifa kubwa ya kuingia
kwenye draw hiyo ni kwa mteja aliyepo au anayejiunga, kuweka akiba ya Shilingi
50, 000 au zaidi.” Alisema Bw. Manongi.
Akifafanua
zaidi Afisa huyo Mtendaji Mkuu wa benki hiyo alisema, kampeni hiyo ambayo
itawawezesha wateja kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali kila mwezi
kwa kipindi cha miezi miwili.
“Mteja
anapoweka akiba (fedha), kiasi cha Shilingi 50,000 au zaidi, atapata alama,
(Point) moja itakayomuwezesha kushiriki kwenye draw.” Alisema.
Alisema,
kadiri Mteja anapoweka akiba zaidi ndivyo Anavyojiwekea nafasi nzuri ya
kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo IPADS na vocha za manunuzi zenye thamani ya
Shilingi 100,000 na kwamba kila itakapochezeshwa draw hiyo, washindi wanane (4)
na kujishindia zawadi mbalimbali.
Akielezea hudma za benki hiyo, Bw.Manongi alifafanua
kuwa Mwalimu Commercial Bank inatoa
gharama nafuu na rafiki za kibenki na ni suluhisho la kifedha kwa walimu,
watumishi wa serikali na wananchi kwa ujumla na kutoa wito kwa Wateja wapya kuja
kufungua Akaunti na kuweka akiba ili wapate nafasi ya kuingia kwenye draw hiyo.
Naye Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko wa Benki
hiyo, Bw. Valence Luteganya alisema, “Huduma za kibenki za MCB ni bora na nafuu, tunawahakikishia wateja wetu waje
kufanya maamuzi ya kifedha yaliyo sahihi kwani tunatoa huduma mbalimbali za
kibenki zilizo nafuu.” Alisema na kuongeza kuwa MCB pia inatoa huduma za ATM
zilizounganishwa na mtandao wa Umoja switch ambao una ATM zaidi ya 200 nchi
nzima.
“Lakini si hivyo tu pia huduma bora za kibenki kupitia
simu za mkononi (Mobile Banking), huduma ya bure ya ujumbe wa SMS ukiwa na
usalama na kuwawezesha wateja kupata taarifa za mara kwa mara kuhusiana na
Akaunti zao. Hivyo natoa wito kwa wananchi kwa ujumla kuja na kujiunga na Benki
yetu kwa huduma bora na za uhakika.” Alisema.
Bw. Manongi akizungumzia kampeni hiyo
Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko wa Benki
hiyo, Bw. Valence Luteganya, akifafanua jinsi kampeni hiyo itakavyofanyika
Meneja Masoko wa benki hiyo, Bi. Rahma Ngassa,(kushoto), akizungumzia ubora wa huduma za kibenki kwenye benki hiyo. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa MCB, Bw. Manongi
Mkutano ukiendelea
Waandishi wa habari wakiwa kazini
Bw. Manongi akisikiliza maswali ya waandishi
Bw. Manongi, (kushoto), akiwa na Bw.Luteganya
No comments:
Post a Comment