NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAAFISA
wa polisi waliokuwa wakishiriki mafunzo ya siku tatu ya polisi Wanawake kutoka
Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika, (SARPCO), wamepata fursa ya kuelewa
kwa undani huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia mada
mbalimbali zilizotolewa na Maafis wa Mfuko huo mwishoni mwa mafunzo hayo kwenye
ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Maafisa
hao waliokuwa wakiongozwa na Mkuu wa Idara ya Uchunguzi wa Kisayansi, (Forensic
Bureau), ya Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi, (CP), Elice Mapunda walipata
fursa ya kujua uendeshaji wa Mfuko huo ambao wanachama wake ni pamoja na
Watumishi wote wa Umma, Sekta binafsi, na watu wote walio katika sekta isiyo
rasmi.
Afisa
Uendeshaji Mwandamizi wa PSPF, Bi.Amina Mtingwa, aliwaambia maafisa hao wa
polisi kuwa, pamoja na kutambua na kusajili wanachama, kukusanya michango na
kutunza taarifa za michango ya wanachama na kuweka michango katika vitega
uchumi mbalimbali.
Alisema,
majukumbu mengine ni pamoja na kulipa mafao kwa wanaostahili kwa mujibu wa
sheria, kutunza kumbukumbu za wanachama na wastaafu, kuangalia upya ubora wa
mafao na kufanya tathmini ya Mfuko na kuweka mikakati.
Aidha
kwa upande wake, Kaimu Meneja Matekelezo wa PSPF, Bi.Ritha M.Ngalo, yeye
alizungumzia mwongozo wa ujumuishaji wa michango (totalization and period of
contribution guidelines 2013) kama ulivyofanyiwa marekebisho kwa polisi
waliochangia GEPF na PSPF.
Aidha
Maafisa hao wa PSPF, walioongozwa na Meneja Huduma kwa Wateja, Bi. Leila
Maghimbi, waliweza kutoa huduma za kuwabadilishia vitambulisho na kuwapatia
vitambulisho vipya baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, lakini pia maelezo
uhusu Mafao yatolewayo na Mfuko katika mpango wa uchangiaji wa lazima, ambayo yamegawanyika
katika makundi mawili ambayo ni Mafao ya huduma za Muda Mfupi kama vile fao la
Uzazi. “Katika kujali ustawi wa wanachama wetu, Mfuko unatoa fao la uzazi kwa
mwanachama mwanamke anapojifungua na dhumuni kubwa ni kumuwezesha kujikimu
kimaisha wakati wa likizo ya uzazi.” Alisema Bi.Leila Maghimbi.
Fao
la Mkopo wa Elimu, Fao la Kujitoa, lakini pia PSPF hutoa Mkopo kwa mwajiriwa mpya
ili kujipanga kimaisha lakini faida nyingine ya anayopata mwanachama ni fursa
ya kupata mikopo ya viwanja, mikopo ya nyumba, mkkopo kwa wastaafu yenye
masharti nafuu.
Aidha
Bi.Maghimbi alsiema, aina ya pili ya Mafao ni Mafao ya Muda Mrefu, ambayo ni
pamoja na Fao la uzeeni, (Old age benefit), Fao la ulemavu, Fao la Mirathi na
Fao la kufukuzwa/Kuachishwa Kazi.
Sambamba
na utoaji wa mada hizo, lakini pia palikuwepo na utoaji elimu wa mtu na mtu
(One to One), ambapo Bi Hawa Kikeke, ambaye ni Afisa Matekelezo Mwandamizi wa
Mfuko, alikuwa akitoa elimu kwa kukutana na mtu mmoja mmoja, huku washiriki hao
waliotoka mikoa yote nchini, ikiwemo Unguja na Pemba, walipata fursa ya kuuliza
utaratibu wa kupata taarifa za michango yao kwa njia ya mtandao na wengine
kuchapishiwa nakala na kuondoka nazo.
Meneja Huduma kwa Wateja, Bi. Leila Maghimbi, akizungumza na washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya Maafisa wa polisi wanawake wa Shirika la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCO), kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Uchunguzi wa Kisayansi,
(Forensic Bureau), ya Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi, (CP), Elice Mapunda, (kulia), akizungumza.
Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PSPF, Bi.Amina
Mtingwa(kulia), akitoa mada.
Kaimu Meneja Matekelezo wa PSPF, Bi.Ritha
M.Ngalo, akitoa mada
Afisa Mwandamizi wa PSPF, Bw. Delphis Richard, (kulia), akimuonyesha Mwanachama huyu michango yake
Mkuu wa Idara ya Uchunguzi wa Kisayansi,
(Forensic Bureau), ya Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi, (CP), Elice Mapunda(kushoto), akimsikilzia Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko huo, Bi. Hawa Kikeke.
Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko huo, Bi. Hawa Kikeke, (katikati), akiwaelekeza namna ya kutumia mtandao wa simu kujipatia taarifa mbalimbali za Mfuko.
Mwendesha mashtaka wa polisi kutoka mkoani Mwanza, Doroth Thomas, (kulia), akiuliza maswali kuhusu michango yake kwa Afisa huyu wa PSPF
Afusa wa PSPF, akiwahudumia wanachama hawa kupata taarifa za michango yao
Afisa wa PSPF, akitoa ufafanuzi kwa wanachama hawa wa Mfuko huo ambao ni maafisa wa polisi
Wasirki wakifuatilia kwa makini
Wasirki wakifuatilia kwa makini
Washiriki wakinakili masuala muhimu yaliyokuwa yakizungumzwa na maafisa wa PSPF
Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PSPF, Bi.Amina
Mtingwa(kulia), akisalimiana na Naibu Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Morogoro, D/RCO, Maria Dominic Kway, (kushoto), huku Bi. Kikeke akishuhudia
Mkuu wa Idara ya Uchunguzi wa Kisayansi,
(Forensic Bureau), ya Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi, (CP), Elice Mapunda(kushoto), Mrakibu wa Polisi, (SP), kutoka idara ya Uhusiano wa Kimataifa Polisi Makao Makuu, Emma Mkonyi, (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko huo, Bi. Hawa Kikeke
Mshiriki akisoma kipeperushi chenye taarifa muhimu za PSPF
Afisa wa polisi akizungumza kwenye mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment