IDARA ya Uhamiaji Mkoani Tanga
imeanza mikakati ya kukabiliana kwa vitendo na wimbi la wahamiaji haramu
kuingia mkoani hapa kwa kuanzisha kizuizi eneo la Mkata wilayani
Handeni kwa muda wa saa 24.
Hayo yalibainishwa na Afisa Uhamiaji Mkoani Tanga DCI, Crispin Ngonyani
wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mipango
waliojiwekea kuzibiti vitendo vya namna hiyo.
Alisema wameamua kuanzisha mpango huo kutokana na asilimia kubwa ya
wahamiaji haramu hao wanapokuwa wamefika kwenye eneo hilo la kizuizi
wanashushwa na kupakia pikipiki maarufu kama bodaboda na kuingia mkoani
Tanga.
“Kutokana na hali hiyo ndio maana tumeamua kuweka kizuizi hicho ambacho
kimekuwa ni eneo ambalo linatumika kuwafaulisha wahamiaji haramu kwenye
pikipiki maarufu kama bodaboda kwa lengo la kuzibiti suala hilo kwa
vitendo “Alisema.
Aidha pia alisema hivi sasa wamejipanga kuhakikisha wanadhibiti maeneo
yote ambayo yamekuwa na mianya ya kutumia kwa ajili ya kupitia ili
kuweza kuhakikisha hawaingii mkoani Tanga.
“Lakini pia tuwatake wananchi kuhakikisha wanawafichua wahamiaji haramu
pindi wanapokuwa wakiwaona kwenye maeneo yao kwani wamekuwa na madhara
makubwa hivyo wanapaswa kutoa taarifa kwa mamlaka husika
“Alisema.
Hata hivyo aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa iwapo watabaini
kuwepo kwa watu wasiowaelewa kwenye maeneo yao ili hatua kali ziweze
kuchukuliwa.
Habari kwa hisani ya Blog ya
Kijamii ya Tanga Raha
No comments:
Post a Comment