Kampuni ya
simu za mkoni ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na GSMA wameandaa mashindano
ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi ambayo yanafanyika
jijini Dar es Salaam kwa mwaka wa pili mfululizo.
Mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na Airtel money
na Comviva wakishirikiana na muungano wa mashirika ya simu za mkononi ulimwenguni
GSMA yanajumuisha washiriki kutoka Africa. Wajasiriamali wa TEKNOHAMA kutoka
Ghana, Kenya, Uganda na Tanzania watachuana kutengeza suluhu kwenye maeneo
makuu matatu, yaani malipo kwenye sekta ya usafirishaji, mfumo wa malipo ya
jumla (bulk payment) na mfumo wa malipo ya pochi ya Comviva na Airtel yaani (
Airtel Comviva mobile wallet).
Tanzania
imepata fursa ya kuandaa mashindano hayo kwasababu inajulikana kama kiongozi
katika sekta ya simu za mkononi inayoongoza katika kujenga mifumo ya malipo ya
simu (mobile money payment) Hivyo ni fursa ya kipekee kwa wajisiriamali wa
kitanzania kuweza kutengeneza suluhu za mifumo ya malipo ya simu za mkononi
zitakazotumika barani Africa.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo,
Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda alisema ushirikiano huu ni
muhimu kwa vile unawezesha wajasiriamali wa TEKNOHAMA kuja na suluhu ambayo
itaweza kusaidia kufanya malipo kupitia simu za mkononi kwa haraka na hivyo
kuokoa kupoteza muda kupanga foleni kusubiria kufanya malipo.
Sisi Airtel Tanzania tumekuwa msitari wa mbele
kuwezesha wajasiriamali kwa njia mbali mbali. Kwa kupitia mashindano
tunaendeleza uwezeshaji huo kwani kwa kila suluhu itakayopatikana haitaishia
hapa mbali itaendelea kuboresha na kuwekwa kwenye mfumo wa malipo ya simu za
mkononi, alisema Nchunda.
Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha Teknohama GSMA
Gareth Pateman alisema washiriki wa mashindano hayo wanaweza kutengeneza suluhi
moja au mbili katika zile tatu huku mshindi akipata ticketi ya kwenda
Barcelona, Spain huku akiwa amelipiwa gharama zote.
No comments:
Post a Comment