Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Airtel bi, Beatrice Singano
Mallya akiongelea mafanikio kya Airtel baada ya na jinsi Airtel ilivyojipanga
kutoa huduma bora zaidi.
· Yasajili
wateja wapya 132,826 kwa kipindi cha miezi mitatu
· Wateja wapya milioni 1.038 wa Airtel Money wasajiliwa
Airtel Tanzania ndio kampuni ya simu za mkononi nchini Tanzania
ambayo imefanikiwa kuongeza wateja wengi kwenye robo ya pili ya mwaka huu huku
makampuni ya simu za mkononi wakishindania kuongeza wateja wapya na watumiaji
wa huduma za kifedha kulingana na ripoti ya Tanzania Communications Regulatory
Authority (TCRA).
Kulingana na ripoti ya robo ya pili ya 2017 (TRCA’s Quarterly Communication
Statistics Report), makampuni ya simu za mkononi Tanzania yaliongeza watumiaji
wapya wa huduma za kifedha 1,059,163 milioni kwa kipindi cha April mpaka Juni.
Kutokana na idadi hiyo, Airtel Tanzania ilisajili wateja wapya
1,038,193. Hii inamaanisha ya kwamba kwa kipindi hicho asilimia 98 ya wateja wa
huduma za kifedha za simu za mkononi wapya waliojiunga na Airtel Tanzania.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio hayo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel
Tanzania Beatrice Singano alisema ‘Hii ni ishara nzuri kuwa Airtel inatoa
suluhisho sahihi kwa huduma za kifedha kwa makampuni ya simu za mkononi hapa
Tanzania. Kwa mfano tuangalie huduma ya mikopo rahisi ya Timiza inayotolewa
kupitia Airtel Money,hatimaye
imeanza kuzaa matunda’.
Huduma ya mikopo ya Timiza inadhihirisha juhudi zetu za kutoa
suluhisho inapokuja suala ya huduma za kifedha kwa kutumia simu za mkononi. Pia
inaenda samba samba na juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa wafanya biashara
wadogowadogo na wakati wanapata huduma ya mikopo yenye marshati nafuu, alisema
Singano.
Ikiwa na ongezeko la 1.038 milioni, Airtel Tanzania kwa sasa ina
jumla ya wateja milioni 5.9 wa Airtel Money kwenye soko ambalo jumla ya
makampuni matano ya simu za mkononi yanashindania wateja milioni 20. Airtel
Tanzania pia imefanikiwa kusajili laini mpya 132,826 kwenye robo ya pili ya
mwaka na hivyo kufikisha jumla ya watejakuwa milioni 10.3. Kwa ujumla, jumla ya
wateja wapya wa simu za mkononi waliongeza na kufikia 40.358 milioni mwishoni
mwa mwezi Juni kutoka 39.856 mwishoni mwa Machi mwaka huu.
Kwa kuendeleza uwekezaji zaidi
nchini kwa mujibu wa Singano anathibitisha kuwa Airtel Tanzania inazidi kukua
vizuri huku kampunihiyo
ikiendelea kuwekeza zaidi kwenye miradi mbali mbali ili kufuta wateja wengi wapya.
Moja ya mradi mkubwa wa uwekezaji ni mradi wa U900.
Kulingana na Singano, Mradi wa U900 unatafuta kuboresha miundombinu ya
kiufundi kwa nia ya kuongeza kiasi cha data na kuboresha kasi ya data
"Hii mikakati yetu ya kuimarisha
maisha ya Tanzania kupitia huduma za kidigitali. Katika jiji la Dar es
Salaam zaidi ya maeneo 300 tayari yamebadilishwa, mpango wetu ni kueneza mradi
wetu wa U900 kwa mikoa ya Mwanza, Morogoro, Dodoma, Arusha na kisha katika
masoko mengine yenye uwezo mkubwa hapa nchini Tanzania, "aliongeza Singano.
No comments:
Post a Comment