Tangazo

September 22, 2017

MPINA AAGIZA KIWANDA CHA UNGA WA NGANO CHA AZANIA KUFANYA VIPIMO VYA VUMBI LITOKALO KIWANDANI HAPO

   Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina akikagua mfereji wa maji katika kiwanda cha Chemi Cotext kilichopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa mazingira.  
    Naibu Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ukaguzi wa mazingira katika eneo la kiwanda cha unga wa ngano cha Azania kilichopo Ubungo jijini Dar Es Salaam jana.
NA EVELYN MKOKOI  - DAR ES SALAAM

Akiendelea na ziara yake ya ukaguzi na utekelezaji wa sheria ya Mazingira jijini Dar es Saalaam, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, ameagiza Baraza la taifa la Usimizi wa Mazingira NEMC kwa kushirikiana na uongozi wa kiwanda cha kutengeneza unga wa Ngano wa Azania, kupima kiwango cha ubora wa hewa inayoambatana na vumbi la unga wa ngano linalotoka kiwandani hapo baada ya shughuli za uzalishaji  na kwenda kwenye mazingira na makazi ya watu kana vinakidhi viwango vya kimazingira.

Mpina alisema kuwa baada ya matokeo hayo  yanayotegemewa kutoka baada ya wiki mbili, serikali ndiyo itakuwa kwenye hatua ya kusema jambo kwa wananchi pamoja na kiwanda.

“Baada ya matokea hayo sasa serikali inaweza kuwa na nafasi ya moja kwamoja kuchukua hatua kwa mwenye kiwanda ikiwa ni pamoja na kukitoza faini kwa mujibu wa sheria, na kama matokeo ya vumbi na kelele zitokazo kiwandani hapo yatakuwa ndani ya kiwango, sasa hatua itakayofuata ni yakuangalia mahusiano kati ya mwenye kiwanda na wakazi majirani wa eneo hilo. Alisema Mpina.”

Aidha Mpina aliongelea kufaanyika kwa taratibu za kujua kama suala la kiwanda hicho kuwa karibu na makazi ya watu ,  ni sahihi na kwa upande wa wananchi kuwa karibu na kiwanda  hususan kuwepo kwa nyumba kila baada ya hatua moja nalo ni sahihi.


Awali  katika muendelezo wa ziara yake ya ufuatiliaji na utekelezaji wa sheria ya mazingira jijini Dar es Salaaam, Naibu Waziri Mpina alikitembelea kiwanda cha Chemi  cotex  kilichopo Mbezi Beach.

No comments: