Tangazo

November 14, 2017

TAMWA YAZINDUA WIKI YA KUADHIMISHA MIAKA 30 TANGU KUANZISHWA KWAKE, MHAVILE ATOA NENO

Mkurugenzi Mtendaji wa Vituo vya ITV, Radio One, Capital TV na Radio, Joyce Mhavile akizungumza jijini Dar es Salaam leo, wakati akizindua wiki ya miaka 30 ya Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA).
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mstaafu, Fatuma Mwassa, akizungumza na wanahabari katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Tamwa, Eda Sanga, akizungumza katika uzinduzi huo.
Wadau mbalimbali na wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo. 


Uzinduzi wa wiki hiyo ukiendelea.


Taswira ya ukumbi wa mikutano ulipofanyika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Tamwa, Eda Sanga, akimvalisha vitengMkurugenzi Mtendaji wa Vituo vya ITV, Radio One, Capital TV na Radio, Joyce Mhavile vilivyo na Tamwa kama zawadi kwake. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mstaafu, Fatuma Mwassa
Mhavile, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo akiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka taasisi mbalimbali.
Ofisa Biashara wa Tamwa, Leonida Kanyuma (kulia), akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Joyce Mhavile kuhusu utendaji wa Tamwa.
Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi (C.R.C), Gladness Munuo akitoa maelekezo kwa mgeni rasmi Joyce Mhavile wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya taasisi mbalimbali kwenye uzinduzi huo.
Mtunza kumbukumbu na Taarifa wa TGNP-Mtandao, Speratus Kyaruzi akitoa maelezo mbele ya mgeni rasmi.
Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shabani Rulimbiye, akimuonesha mgeni rasmi moja ya vipeperushi vya shirika hilo cha  kupinga ukatili wa kijinsia.
Mhavile akizungumza na wajasiriamali wakati alipotembelea mabanda yao.


Suleiman Msuya

WANAWAKE nchini wametakiwa kuonesha uwezo katika nafasi wanazozipata na kauchana na dhana ya kupata upendeleo au kubebwa kama inavyotafsiriwa na jamii.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Vituo vya ITV, Radio One, Capital TV na Radio, Joyce Mhavile wakati akizindua wiki ya miaka 30 ya Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) leo asubuhi jijini Dar es Salaam.

Mhavile alisema wanawake wengi wanaonesha kushindwa kufikia malengo yao katika nafasi mbalimbali ambazo wanapata kuzitumikia kutokana na kuishi na dhana kuwa watapewa upendeleo fulani.

Alisema tatizo hilo lipo kwa wanawake wa makundi yote wakiwemo waaandishi wa habari wafanyabiashara na makundi mengine ambayo yanabakia kulalamika.

“Mi nasema hivi ukipata nafasi katika dunia hii itumie kwa kuonesha uwezo wako ili watu watambue kipaji chako na si kutegemea kubebwa au upendeleo fulani kisa wewe mwanamke hiyo si sawa,” alisema.

Mhavile ambaye alizindua wiki hiyo ikishirikisha maonesha mbalimbali aliwataka wanawake ambao wanashiriki maonesho hayo kutumia vyombo vya habari kujitanga ili bidhaa zao ziweze kufahamika.

Mkurugenzi huyo alisema iwapo kila mwanamke ataondokana na dhana ya kuwezeshwa ni dhahiri kuwa watafanikiwa kwa haraka hivyo ubunifu kwa kila wanalofanya ni muhimu kwa sasa.

Alisema TAMWA inapaswa kupanua wigo zaidi katika shughuli wanazofanya ili kufikia jamii kubwa kwani changamoto zilizopo ni nyingi na zinahitaji utatuzi.

“Ukipata nafasi katika dunia hii ichukue na uishughulike pia uwe mwepesi kubuni mbinu mbalimbali ili kufikia malengo kwa haraka naamini tutafikia malengo,” alisema.

Alisema vyombo vya habari vinapaswa kuwajibika kwa jamii kwa kuandika habari ambazo zinaonesha matokeo chanya kwa kila kinachofanywa na wanawake.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tamwa, Eda Sanga alisema chama chao kinaazimisha miaka 30 kikiwa kimefanikiwa kutoa mafunzokwa zaidi ya waandishi wa habari 2,000 hali ambayo imechochea uandishi wa masuala ya  jinsia kupata nafasi katika vyombo vya habari.

Alisema mikakati yao ni kuhakikisha wanatumia kioo walichonacho kumulika changamoto za unyanyasaji wa kijinsia katika jamii.

Sanga alisema pamoja na mafunzo pia wamekuwa wakitoa ufadhili kwa waandhishi wa habari ili kwenda kwenye jamii iliyoathirika na unyanyasaji wa kijamii kuibua changamoto.

“Miaka 30 hii ni ya mafanikio sana kwetu kwani tumefanikiwa kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari 2,000 ambao wamekuwa mabalozi wazuri katika kuibua habari za unyanyasaji wa kijamii na matarajio ni kuendelea kuwajengea uwezo zaidi,” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema unyanyasaji wa kijinsia mfumo rithiwa tangu huko zamani ila wakati muafaka umefika kwa jamii yote kushirikiana ili kufikia katiia mfumo rafiki na shirikishi kwa kila mtu.

Alisema kwa sasa hakuna haja ya kundi fulani kulaumu kundi lingine ila kinachohitajika ni jamii kujua kuwa uwasa wa kijinsia ni muhimu kwa maendeleo ya nchi na wananchi.

No comments: