. Gawio la Airtel Money kwa wateja
lafikia bilioni 14.8
Airtel Tanzania imetoa gawio
linalofikia shilingi bilioni 14.8 hadi sasa kwa wateja wake na mawakala nchi
nzima ikiwa ni sehemu ya faida waliyoipata tangu mwaka 2015.
Hili limebainishwa na Mkurugenzi wa
masoko wa Airtel Tanzania, Isack Nchunda kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Airtel
wakati akitangaza gawio la robo hii ambalo ni shilingi bilioni 1.8.
“Tangu tuanze kugawa sehemu ya
faida yetu kwa wateja mwaka 2015, tumeshatoa jumla ya shilingi bilioni 14.8 na
huwa tunagawa kila robo ya mwaka na kuhakikisha wateja na mawakala wanapokea
fedha hizi kupitia akaunti zao za Airtel Money na wana uhuru wa kutumia fedha
hizi wanavyotaka,” alisema.
Kwa mujibu wa Nchunda, hii ni mara
ya sita mfulululizo kwa Airtel Tanzania kugawa sehemu ya faida kwa wateja wake
tangu mwaka 2015. “Bwana Pesa hutoa gawio hili kwa wateja wa Airtel Money na
mawakala kulingana na salio la mteja kila siku,” aliongeza.
Aliwashukuru wateja wa Airtel kwa
kuendelea kutumia Airtel Money na kuifanya iwe huduma yenye tija na maarufu
zaidi na kuongeza kuwa hadi sasa wana zaidi ya maduka 100 maalum kwa kutoa
huduma ya Airtel Money ambayo yanafanya huduma hii iwe ya kuaminika zaidi
na rahisi kupatikana.
“Maduka haya ya Airtel Money
huhakikisha mawakala wana salio la kutosha muda wote ili wateja wasipate
usumbufu wanapohitaji huduma hiyo,” alisema.
Kwa upande wake, Meneja wa Airtel
Money, alisema kuanzia leo, wateja wa Airtel Money na mawakala watapata gawio
linalofikia shilingi bilioni 1.8 kupitia akaunti zao za Airtel Money na
wanaweza kutumia gedha hizo wanavyotaka ikiwemo kulipia huduma mbalimbali kama
vifurushi vya mtandao, muda wa maongezi na LUKU.
Alitoa wito kwa mawakala wa Airtel
Money kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa wateja ili kampuni hiyo
iendelee kutoa gawio kwa wateja wake kila robo ya mwaka.
“Airtel Money imejizatiti kuendelea
kutoa huduma bora na nafuu ambayo ni suluhisho kwa biashara za aina yoyote,”
alisema na kuongeza kuwa Airtel inashirikiana na biashara zaidi ya 400 na ziadi
na benki 30 katika kutoa huduma za kifedha.
Airtel ina zaidi ya mawakala 50,000
nchi nzima na inaendelea kutanua wigowake ili kuhakikisha huduma za kifedha
zinapatikana katika miji na vijijini.
Airtel Money Announces disbursement of Tsh 1.8bn Interest this
quarter
- Airtel Money
Interest to customers reach Tsh 14.8 bn
Airtel Tanzania has so far disbursed Airtel Money Interest
amounting to Tsh 14.8 billion to its Airtel Money customers countrywide, making
it one of the most consistent and regular arrangement.
This was revealed by the Airtel Marketing Director, Isack Nchunda
on behalf of Airtel Managing Director while announcing this quarter’s interest
which amounts to Tsh 1.8bn.
“Since we started December 2015 we have so far disbursed to our
customers who also include Airtel Money agents Tsh 14.8 billion and we announce
and make these disbursements every quarter where customers receive their money
through their Airtel Money accounts and they have the freedom to decide how to
spend the money,” he said.
According to Nchunda, this is the sixth time consecutively Airtel
is giving back interests to all Airtel Money customers and agents since 2015.
“Mr. Money gives back to Airtel Money customers and agents depending on the
amount of balance one has on Airtel Money account on daily basis,” he added.
He also thanked their customers for their loyalty to the Airtel
Money service which has become popular countrywide as there are over 100 Airtel
Money shops rollout countrywide which makes it more reliable and easily
accessible.
“The shops are there to ensure that the agents have enough float
at all times to ensure customers are not inconvenienced when they visit the
agents,” he said.
On his part, Airtel Money Manager Ibrahim Malando said starting
today every Airtel Money customers and agents countrywide will receive
part of Tsh 1.8bn interest through their Airtel Money accounts and one
can decide to use the money to either cash it out, paying various bills
and services such as internet bundle, purchase Airtel time, LUKU and so on.
He called on Airtel Money agents to continue offering the best
services to customers to ensure the dividends continue increasing in the coming
quarters.
“Airtel Money is committed to offer the most affordable mobile
money services offering payment solution to businesses of any form,” he said
adding that Airtel has also integrated with more than 400 Businesses and over
30 banks for easy payment solutions model and instant cash transfer activities.
With more than 50,000 Airtel Money Agents county wide Airtel
continues to widened it agent’s footprint to ensure mobile money services
availability to majority Tanzanians in both rural and urban areas.
No comments:
Post a Comment