Tangazo

January 24, 2012

BUS LA NEW FORCE LAUA STENDI YA MABASI MBEYA




ABIRIA aliyefahamika kwa jina moja la Amina mkazi wa wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya alikufa papo hapo katika ajali iliyotokea juzi usiku  katika Kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani jijini Mbeya baada  ya Bus la New Force kuparamia ukuta wa mgahawa uliopo mkabala na Ofisi za Mabasi ya Kampuni hilo.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 5:00 usiku wa Ijumaa ya Januari 20 mwaka huu  katika Kituo hicho cha Mabasi yakitokea mikoa mingine.

Mashuhuda wa tukio hilo, wamesema kondakta wa basi hilo aliyejulikana kwa jina la Januari Kapinga aliingia ndani ya basi hilo lenye namba za usajili T 853 AVQ aina ya Yutong lililokuwa likitokea Dar es Salaam baada ya abiria wote kushuka ndipo alipolikurupua kwa nguvu na kumshinda hatimaye kuparamia ukuta.

Abiria aliyefariki alikuwa safarini kuelekea masomoni mkoani Tabora na wakati gari likiparamia ukuta wa mgahawa huo alikuwa akipata chakula cha jioni

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema licha ya mmoja huyo kupoteza maisha, lakini watano wamejeruhiwa.

Aidha kondakta wa basi hilo, alitoroka na kwenda kusikojulikana na juhudi za Jeshi la Polis kumtafuta zinaendelea na hadi sasa dereva wa basi hilo anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano zaidi.
Picha na Habari kwa Hisani ya Mbeya Yetu Blog

No comments: