Mratibu
wa Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga Latiba Ayoub akizungumza
wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo ya siku moja iliyokuwa na lengo la
kujaribu kujadili changamoto kwenye
sheria za mtoto na kanunuzi zake hususani waliopo kwenye ukinzani nazo
wakiwemo kama wadau iliyofanyika mjini hapa
Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (Tawla)
Mwanaidi Kombo akizungumza wakati wa warsha hiyo ya siku moja
iliyofanyika ukumbi wa YDCP Jijini Tanga
Afisa wa Dawati Jeshi la Magereza mkoani Tanga ASP Halima Mswagilla akichangia jambo kwenye warsha hiyo |
Wakili wa Serikali Rebbeca Msalangi akisisistiza jambo kwenye warsha hiyo wakati akiwasilisha mada |
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwang’ombe Jijini Tanga Husna Abdi wa pili
kutoka kulia akichukua baadhi ya dondoo kwenye warsha hiyo
SERIKALI
imeshauriwa kujenga mahabusu za watoto kwenye mikoa na wilaya hapa
nchini ili kuwaweka watoto waliokuwa katika ukinzani wa kisheria ambao
wamekuwa wakifanya vitendo viovu.
Hatua hiyo itakuwa sehemu ya
kuwaweka watoto happy wakiwa wanasubiri kesi zao kusikilizwa badala ya
ilivyokuwa hivi sasa watoto hao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto
mbalimbali kutokana na uhaba uliopo.
Hayo yalisemwa juzi na
Mratibu wa Chama cha Wanasheria wanawake mkoani Tanga (TAWLA) Latifa
Ayoub wakati wa warsha ya siku moja iliyokuwa na lengo la kujaribu
kujadili changamoto kwenye sheria za mtoto na kanunuzi zake hususani
waliopo kwenye ukinzani nazo wakiwemo kama wadau iliyofanyika mjini hapa
Alisema kutokana na uhaba wa mahabusu za watoto wamekuwa wakati
mwengine wakikumbana na changamoto kadhaa wakati wakisubiri utaratibu
wa kusikilizwa kesi zao wanazokabiliana nazo kabla ya kutolewa hukumu.
“Hivi
sasa kuna watoto wanakuwa kuzidi umri wao na wanafanya vitendo viovu
huku wazazi wakiwa hawana uwezo hivyo kupelekea wimbi lao kuwa wengi na
mahabusu yao ni chache hivyo kuna umuhimu wa serikali kuliangalia jambo
hili kwa mapana kwa kuziongeza angalau mkoa na wilaya “Alisema
Hata
hivyo alisema pia sehemu hizo ambazo watakuwa wakiwekwa watoto hao
itakuwa ni eneo ambalo watakaa wale ambao wapo kwenye ukinzani wa
kisheria wakisubiri hitimisho la kesi zao ambazo wanatuhumiwa kuhusika
nazo.
Naye kwa upande wake Hakimu Mkazi wa Mahakama ya
Mwang’ombe Jijini Tanga Husna Abdi alisema watoto wanaokinzana na sheria
wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kuchanganywa na watu wazima
watoto kutokupewa haki zao.
Alisema kupitia warsha hiyo ambayo
wamekutana wadau mbalimbali wakiwemo ustawi wa Jamii,Jeshi la
Polisi,Mahakamani wawe chachu ya kuielimisha jamii kuhusu haki zao ili
kuhakikisha haki inatendeka vema kwa mujibu wa sheria.(Habari kwa
Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)