Tangazo

September 26, 2011

KAMPUNI ZA BIO RAD NA PYRAMID PHARMA LTD ZAWAKUTANISHA WATAALAM WA MAABARA NA MAMENEJA MIPANGO YA DAMU SALAMA - AFRIKA

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, D. Margaret Mhando akifungua mkutano wa wadau wa vifaa na mitambo ya kupimia magonjwa mbalimbali yanayotokana na virusi vinavyoambukizwa kupitia kuongezewa damu na vitenganishi vya makundi ya damu uliowashirikisha wataalamu wa maabara na mameneja mipango ya damu salama kutoka nchini mbalimbali za Afrika, uliofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Mkutano huo uliondaliwa na Pyramid Pharma Ltd ambao ni Wakala wa Bio Rad Laboratories (Pty) Ltd ya Afrika Kusini. PICHA ZOTE/DAILY MITIKASI BLOG
Meneja wa Bio Rad Kusini Mwa Afrika, Ronald Shumba ndiye aliyekuwa Mwongozaji wa mkutano huo.
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo.
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo akingalia damu isiyo salama wakati walipotembelea Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Mashariki zilizopo katika eneo la Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam.
Mtaalam wa Maabara wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Mashariki, Sam Mduma (wa pili kushoto) akitoa maelezo wa washiriki hao.
Baada ya kutembelea Mpango wa Damu Salama kule Ilala, washiriki wa mkutano huo walimalizia ziara yao katika Maonyesho ya 15 ya Kimataifa ya afrika Mashariki 2011 yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo walitembelea banda la kampuni ya BIO Rad Laboratories (Pty) Ltd na kupata maelezo kuhusu vifaa mbalimbali vinavyotumika kupimia damu katika maabara.
Mtaalam kutoka BIO RAD, Mohamed Shafiek Shaikjee akitoa maelezo.

No comments: