Tangazo

September 23, 2011

KUNDI LA TAARAB LA T-MOTO KUWANG’ALISHA MASHABIKI WAKE KWA PAMBA ZA T-MOTO





KUNDI jipya la Taarab la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) linalotarajia kuzinduliwa Oktoba 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam, limezindua mavazi yake rasmi kwa ajili ya kuwazawadia mashabiki wake siku ya uzinduzi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kundi hilo, Amini Salmini, alisema kuwa wameamua kuandaa Tisheti kwa ajili ya wanaume na Vitop vya Kidada, zenye Nembo ya kundi hilo kwa ajili ya mashabiki wa kundi hilo, watakaojitokeza kushudia uzinduzi wao.

Aidha Amini alisema kuwa Ujio wa kundi hilo utakuwa ni tofauti na makundi mengine yaliyopita kutokana na kujiandaa vilivyo na kulifanya kundi hilo kuwa ni la kipekee katika utendaji kazi na kujali maslahi ya kila msanii wa kundi hilo.

“Kwanza kabisa kundi langu nimeangalia zaidi maslahi ya wasanii na kufanya utafiti ni vitu gani wanapendelea zaidi wasanii ili kuweza kufanya kazi kwa bidii na kujituma zaidi, nikaona la kwanza ni maslahi ambayo ndiyo kitu cha kwanza kufanyia kazi na kujipanga zaidi.
 
 Na pia ili kumfanya msanii aweze kuinjoi na kuipenda kazi yake ni lazima awe na mazingira mazuri ya kufanyia kazi ikiwa ni pamoja na vyombo vizuri, ambalo pia nimelipa kipaumbele kwa kuanzisha kundi nikiwa tayari nina vyombo vilivyokamilika na kuongeza ufanisi zaidi kwa kuongeza Gitaa la tatu la rythim jambo ambalo makundi mengine hayajafanya hivyo” alisema Amini

Alisema kuwa ameweka magitaa matatu katika kundi hilo ili kuweza kuongeza radha ya muziki na kuleta uotafauti baina ya nyimbo za kundi hilo na nyimbo za makundi mengine.

No comments: