|
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akifafanua jambo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari juu kupanga ratiba ya fainali za Taifa za michuano ya Airtel Rising Stars ambayo inatarajiwa kuanza Jumamosi hii kwenye uwanja wa Kumbu Kumbu ya Karume Dar es Salaam, zikishirikisha timu za kombaini za Mwanza, Iringa, Morogoro na Dar es Salaam. Katikati ni Afisa Habari wa TFF Boniface Wambura na Afisa Mashindano hayo, Iddi Mshangama. Upangaji ratiba huo ulifanyika kwenye ofisi za TFF, Dar es Salaam jana. |
********************************************
Wachezaji sita kuchaguliwa kujiunga na kliniki ya Manchester United
Kikosi cha timu ya mwanza cha vijana chini ya umri wa miaka 17 watapambana vikali na kikosi cha timu ya morogoro katika mashindano ya kusisimua ya Airtel Rising Star yatakayoziduliwa na kuchezwa katika viwanja vya karume siku ya Jumamosi Dar es salaam huku wenyeji kikosi cha timu ya Dar es Salaam kikijiandaa kuchuana Iringa siku JumapiliDroo ya kupanga mechi za fainali ilifanyika Jumatano 14 septemba 2011 katika ofisi za TFF jijini Dar es Saalam ambapo Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando aliwapa changamoto wachezaji kuonyesha uwezo wao wa kulisakata kandakanda ili waweze kuonekana na kuchaguliwa na kikosi cha ufundi toka TFF na kuwa kati ya wachezaji sita bora watakaoingia clinicWachezaji sita bora watapata nafasi ya kuingia katika cliniki itakayoendeshwa na wajuzi wa soka kutoka manchesta na kupata mafunzo, washindi hao watakuwa kambini na washiriki wengine kutoka nchi za jirani kama Kenya, Uganda, Malawi and Sierra Leone. AliongezaZaidi yawashindi bora watakaochaguliwa mashindano ya Airtel Rising Star yatatoa zawadi mbalimbali kwa shule zilizoshiriki ikiwemo vitabu vya masomo ya sekondari ambayo vitawasaidia katika kuinua viwango taaluma mashuleniMmbando aliongeza kwa kusema tunagetemea kupokea timu kutoka mikoani kuanzia Alhamisi, 15 Septemba 2011. Matayarisho ya malazi, chakula na vifaa vya michezo kwa timu zote yamekamilika
Akiongelea kuhusu cliniki hiyo ya Manchesta united Mmbando aliongeza kwa kusema, ni ya kiwango cha hali ya juu na itakayowapatia vijana mafunzo bora na ya kiwango cha juu ambayo itaanza Rasmi tarehe 30 october 2011 hapa Dar es Saalam.
No comments:
Post a Comment