Tangazo

September 6, 2011

Rais Dk. Jakaya Kikwete aipongeza NSSF

Rais Dk. Jakaya Kikwete akikabidhi cheti cha mchangiaji bora wa sekta ya ujenzi kwa wazawa kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau.
Rais Dk. Jakaya Kikwete jana amemkabidhi Cheti Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dr. Ramadhani Dau kwa kutambua mchango mkubwa wa Mfuko huo katika sekta ya ujenzi hapa nchini.

Rais Kikwete ambaye alikuwa mgeni kwenye ufunguzi wa Mkutano wa siku tatu uliojumlisha Wahandisi, Wabunifu Majengo, Wakadiriaji na Makondrasi alitoa zawadi hiyo kwa niaba ya Bodi ya Wakondrasi.

Mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya watu, kutoka nje na ndani, ulianza tarehe 5 na utakwisha tarehe 7 Septemba mwaka huu. Baadhi ya wajumbe walitoka Afrika Kusini, Zambia, Kenya na Malawi.
 
Akiongea kwenye hafla hiyo fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City mjini Dar es Salaam, Rais aliwapongeza Wahandisi, Wabunifu Majengo, Wakadiriaji na Makondrasi walioandaa mkutano huo na kuwataka wajiunge pamoja ili waweze kupata uwezo mkubwa wa kufanya kazi.

Katika siku za karibuni NSSF imekuwa na miradi mikubwa ya ujenzi. Baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, nyumba za Polisi Dar es Salaam na Zanzibar na nyumba za Jeshi huko Monduli Arusha. Hivi karibuni NSSF itaanza kujenga Daraja la Kigamboni.

No comments: