Tangazo

September 22, 2011

Rais Kikwete katika Soko la Hisa la NASDAQ jijini New York

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na baadhi ya wake wa Marais wa nchi za Afrika, Mawaziri wa Afya na viongozi wa afya pamoja na maofisa wa juu wa soko la Hisa la NASDAQ wakishangilia baada ya Rais Kikwete kugonge kengele kuashiria mwisho wa shughuli za soko hilo kwa siku ya Jumatano Septemba 21, 2011 makao makuu ya NASDAQ barabara ya 4 eneo la Times Square jijini New York.

Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii wa Zanzibar Mh Juma Duni Haji (kulia) na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa Tanzania Bara, Dk. Hadji Mponda wakisalimiana na Balozi wa Heshima wa Roll Back Malaria na Mwinbaji mashuhuri wa Afrika ya Kusini, Yvonne Chaka Chaka makao makuu ya soko la Hisa la NASDAQ Jumatano Septemba 21, 2011 barabara ya 4 eneo la Times Square jijini New York. Hii ilikuwa ni kabla ya kuanza kwa mjadala wa umuhimu wa ushirikiano wa taasisi za umma na binafsi katika kushughulikia afya ya mwanamke (Public Private Partnership for women's health ulioandaliwa na taasisi ya Viongozi wa Afya wa Dunia.

Rais Jakaya Kikwete akishiriki katika mjadala wa umuhimu wa ushirikiano wa taasisi za umma na binafsi katika kushughulikia afya ya mwanamke (Public Private Partnership for women's health ulioandaliwa na taasisi ya Viongozi wa Afya wa Dunia katika makao makuu ya soko la Hisa la NASDAQ  baada ya Rais Kikwete kugonge kengele kuashiria mwisho wa shughuli za soko hilo kwa siku ya Jumatano Septemba 21, 2011 makao makuu ya NASDAQ barabara ya 4 eneo la Times Square jijini New York.PICHA/IKULU

No comments: