Tangazo

September 22, 2011

RAIS KIKWETE KATIKA MKUTANO WA UN

Rais Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Luxembourg Mheshimiwa Jean Asselborn wakati wa kikao cha 66 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York nchini Marekani juzi.

Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Rais wa Slovenia Dr. Danilo Turk kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York juzi. Viongozi hao wanahudhuria kikao cha 66 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilichoanza juzi.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihudhuria mkutano wa 'Social Good Summit' na kupokea tuzo kutoka United Nations Foundartion for his work in Martenal Health and Social Media Commitment kutoka kwa Makamu wa Rais wa Public Policy of United Nations Foundation Mr. Peter Yeo katika sherehe fupi iliyofanyika jijini New York juzi.

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki- Moon kwenye Makao Makuu ya Umoja huo jijini New York nchini Marekani juzi. PICHA ZOTE NA JOHN LUKUWI 

No comments: