Tangazo

September 12, 2011

TBL YAJENGA KISIMA CHA MILIONI 9/- KATIKA KITUO CHA AFYA YA UZAZI MBAGALA

Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kulia) na Rais wa Rotary Club Mikocheni, Irene Kamau wakikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi kisima cha maji chenya matanki mawili ya kuhifadhi lita 10,000 za maji kwa Kituo cha Afya ya Uzazi cha Mbagala Round About, Temeke, Dar es Salaam juzi. Anayeshuhudia (kushoto) ni Daktari Mkuu Mfawidhi wa kituo hicho, Batuli Luhanda. Kupitia Rotary hiyo TBL ilifadhili mradi huo kwa gharama y ash. Milioni 9.

Wanachama wa Rotary Club Mikocheni, wakiongozwa na Rais wao, Irene Kamau ( wa pili kulia) wakimshukuru Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kushoto), baada ya ya kukabidhi kwa Kituo cha Afya ya Uzazi cha Mbagala Round About, Temeke Dar es Salaam juzi. Mradi wa kisima cha maji chenye matanki mawili ya kuhifadhi lita 10,000 kilichojengwa kwa ufadhili wa TBL kwa gharama ya sh. Milioni 9. (Wa pili kushoto ni Daktari Mkuu Mfawidhi wa kituo hicho, Batuli Luhanda.

No comments: