Mkufunzi kutoka Veta Kanda ya Mashariki na Kati, Marthin Mollel
akitoa mafunzo ya ujasiliamali ya airtel fursa kwa vijana yenye lengo la kuwapa
elimu ya usajiliamali ili kujiendeleza kibiashara na kujikimu kiuchumu
yakishirikisha vijana 250 wenye umri wa kuanzia 16 hadi 26 na kufanyika ukumbi
wa Veta mkoani Morogoro.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
· Vijana
moro wachangamkia mradi wa Airtel Fursa wiki hii
Morogoro
VIJANA zaidi ya
200 mjini Morogoro wamehudhuria warsha ya siku nzima ya 'Airtel FURSA Tunakuwezesha.
Airtel Fursa ni mpango unaowalenga vijana wemye umri kati ya miaka 18 -24 na
wanamiliki biashara ndogo ndogo kwa kuwapatia ujuzi na nyenzo muhimu kwa
mafanikio ya biashara zao na kuweza kujenga fursa kwa wengine.
Akizungumza
katika warsha hiyo, mmoja wa washiriki bw. Musa Ndauka alisema;"napenda
kuwashukuru Airtel kwa kutambua changamoto ambazo vijana tunakumbana nazo
katika maisha yetu ya kila siku. Sisi vijana tupo tayari kufanya kazi kwa bidii
ili kufikia malengo yetu lakini hatuna ujuzi muhimu na zana ili kujenga
biashara zetu. Airtel imeliona tatizo hili na kuchukua jukumu hili na
kutusaidia sisi vijana wa Morogoro"
"Leo hii tumepata stadi za msingi za
ujasiriamali, nimejifunza umuhimu wa kutunza kumbukumbu bila kujali udogo wa
biashara yangu. Sasa hivi ninajua jinsi ya kuweka vitabu yangu vya akaunti,
jinsi ya kutafuta soko la bidhaa zangu hasa kwa kutumia teknolojia ili niweze
kufikia wateja zaidi. Kwa kifupi, warsha hii imekuwa mwangaza wa mafanikio wa
maisha yangu. "aliongeza Ndauka
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa warsha hiyo afisa masoko wa Airtel Tanzania,
Aminata Keita, alisema "tunaelewa changamoto nyingi ambazo vijana wamekuwa
wakikutana nazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira. Nchini Tanzania, vijana
wapatao milioni moja kila mwaka huwa wanapata matatizo ya ajira. Tunahitaji
kuwawezesha na kubadili mawazo ya kutaka kuajiriwa kwa kuwasaidia kuwa
wabunifu na kuweza kujiajiri. Mpaka sasa Airtel
FURSA Tunakuwezesha imewawezesha
vijana zaidi ya 1200 kupitia warsha hii na tuna mpango wa kufikia vijana
wapato 2000 mwaka huu peke yake. Tunatambua na kuwapongeza hawa vijana ambao ni
wafanyabiashara wadogo wadogo kwa juhudi walizofanya na kuweza kufikia
hapa walipo licha ya changamoto hizi zote. Nami nawahimiza vijana
kujitokeza kwa wingi na kuomba kuwezeshwa kupitia mradi wa “Airtel FURSA Tunakuwezesha”,
"alisema Keita
Alitoa
wito kwa vijana katika mkoa wa Morogoro kutumia nafasi hii ya “Airtel FURSA
Tunakuwezesha” kwa kuweza
kujiendeleza kibiashara na kuhakikisha kuwa wanapanuka kibiashara. Morogoro ina
mambo mengi mazuri sana kwahiyo vijana watumie mji wao kuweza kujiendeleza na
vile vile kupanua uchumi wa Morogoro. Huu sio muda wa kukaa bila kazi wakati
kuna fursa inayokuwezesha kupata maarifa ya bure. Vijana wetu lazima
wajishughulishe na vitu tofauti vitakavyowawezesha kushiriki katika shughuli
mbalimbali zitakazowafanya wafaidike na kuweza kujikomboa na umasikini,
"alisema Keita
Alisisitiza
kwamba mpango wa “Airtel FURSA Tunakuwezesha” unawalenga wale vijana ambao
tayari wanabiashara na walio katika umri kati ya miaka 18-24, na
anayeishi Tanzania na kuendesha biashara zake hapa nchini. Ili kijana kushiriki
au kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba
15626 au barua pepe kwaairtelfursa@tz.airtel.com au kutembelea mtandao wa
Airtel na kurasa za kijamii kwa maelezo zaidi.
Keita
alihitimisha kwa kusema Airtel imedhamiria kufanya kazi na Serikali ili kusaidia
kuwajenga vijana na kuwaweka kuweza kuamini kwamba Airtel
FURSA Tunakuwezesha' ipo kwa
ajili yao na kuleta mabadiliko na msisimko kwa vijana mkoani Morogoro na
maeneo mengine ya hapa nchini.
No comments:
Post a Comment