Mtoto Careen Modest Kassuw pichani, ana umri wa mwaka mmoja, amezaliwa ana tatizo la Moyo ukiwa na matundu mawili na valvu zake nyembamba zimebana kiasi hivyo analazimika kusafirishwa kwenda India kwa matibabu.
Wazazi wa mtoto huyo wanaomba msaada wako wewe Mtanzania kwa atakayeguswa ili wafanikishe gharama za matibabu ya mtoto Careen ambayo ni Shilingi Milioni 30 zinahitajika ili kuokoa maisha yake.
Ewe Mtanzania, ewe mzazi tunaomba mchango wako wa hali na mali, kwa atakayeguswa tunaomba utume mchango wako kwa mama mzazi wa mtoto huyo Eunice kwa namba 0713 034866 au kwa namba 0715 083055
Mungu awabariki wote mtakaochangia kwa njia moja au nyingine.
No comments:
Post a Comment