Tangazo

May 28, 2014

MAMIA WAMZIKA PAPARAZI MAX JOHN NGUBE

Waandishi wa Habari wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mpigapicha wa Mlimani TV, Marehemu Maxmillian John Ngube, wakati wa hafla ya kumuuaga iliyofanyika katika viwanja vya Klabu ya Leaders jijini Dar es Salaam jana na baadaye mazishi kufanyika katika makaburi ya Kinondoni. Marehemu Max alifariki Mei 23 mwaka huu kwa maradhi ya Sukari na Presha, ameacha mke na watoto watano. PICHA NA JOHN BADI wa Daily Mitikasi Blog
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akitoa heshima za mwisho.
Wasanii wa Bongo Movie na Wanamuziki kutoka Bendi Mbalimbali walihudhuria.
Mtoto wa Marehemu Max, Jacob akilia kwa uchungu wakati akiuaga mwili wa baba yake.
Mtoto wa Marehemu Max, Rose akilia kwa uchungu wakati akiuaga mwili wa baba yake.

Mjane wa Marehemu, Bi. Suzan Jacob Ayimba akiuaga mwili wa mpendwa mme wake.
Jeneza lenye mwili wa Marehemu Max (pichani) likiondolewa katika viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kupelekwa katika makaburi ya Kinondoni kwa Mazishi.
Jeneza lenye mwili wa Marehemu Maxlikiwekwa juu ya kaburi kabla mazishi.
Mjane wa Marehemu, Bi. Suzan Jacob Ayimba akiweka udongo kwenye kaburi la  mpendwa mme wake.
Mtoto wa Marehemu Max, Jacob akisaidiwa baada ya kupoteza fahamu wakati akutupia udongo kwenye kaburi la baba yake.
Mjane wa Marehemu, Bi. Suzan Jacob Ayimba akiweka shada la maua kwenye kaburi la mume wake.
Watoto wa Marehemu, wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao.

No comments: