Tangazo

October 26, 2011

AIRTEL RISING STARS YAJA TENA

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya (katikati) akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari zaidi ya 20 juu ya awamu ya nne ya  Airtel Rising Stars Football Clinic itakayo fanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam chini ya  udhamini wa Makocha wa timu ya Manchester United. Zoezi hilo litakalo anza Oktoba 30 hadi Novemba 3 mwaka huu, litawahusisha vijana wadogo kutoka nchi za  Kenya, Malawi, Sierra Leone na Tanzania. Pamoja nae ni Ofisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde (kushoto) na Msimamizi wa Fedha wa AON Deepna Shah.

Wahariri wa Habari za michezo kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya wakati alipokuwa akizungumza nao juu ya awamu ya nne ya  Airtel Rising Stars Football Clinic itakayo fanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaamtchini ya  udhamini wa Makocha wa timu ya Manchester United. Zoezi hilo litakalo anza Oktoba 30 hadi Novemba 3 mwaka huu, litawahusisha vijana wadogo kutoka nchi za  Kenya, Malawi, Sierra Leone na Tanzania.

Mmoja wa Wahariri wa Habari za Michezo Salehe Ally wa Global Publishers Limited akichangia mada wakati wa mjadala maalumu baina ya wahariri wa Habari za michezo zaidi ya 20 walipokutana na maofisa wa kampuni ya simnu ya Mkononi ya Airtel jijini Dar es Salaam jana.



No comments: