Tangazo

October 12, 2011

MAKAMU WA RAIS, DKT. BILAL ATOA POLE MSIBA WA MTOTO WA MWAPACHU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Kitabu cha maombolezo cha Harith Mwapachu, ambaye ni mtoto wa Juma Mwapachu, aliyefariki dunia jana. Kulia ni Balozi Juma Mwapachu. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mke wa Balozi Juma Mwapachu, Rose Mwapachu, wakati alipofika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam leo jioni kumpa pole kufuatia kifo cha mtoto wake, Harith Mwapachu kilichotokea jana Oktoba 11, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Freeman Mbowe, wakati walipokutana katika msiba wa mtoto wa Balozi Juma Mwapachu, Harith Mwapachu nyumbani kwa Mwapachu Mikocheni jijini Dar es Salaam jana Oktoba 11. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Sir. George Kahama  wakati akiondoka nyumbani kwa Balozi Juma Mwapachu, wakati alipofika kutoa pole kufuatia kifo cha mtoto wa Balozi Juma Mwapachu, Harith Mwapachu jana Oktoba 11. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments: