Tangazo

October 11, 2011

Uzinduzi wa Kituo cha Afya cha Mt. Benedikt Kitunda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadik akikata utepe kuzindua Kituo cha Afya cha Mt. Benedict kilichopo kata ya Kitunda Manispaa ya Ilala hivi karibuni. Kituo hicho kinamilikiwa na Masista wa Shirika la Wabenedict la  Mt. Agnes lenye makao yake makuu Chipole Songea.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwa kwenye picha ya pamoja  na watumishi wa Kituo cha Afya cha Mt. Benedict  baada ya kukizindua rasmi. Waliokaa kulia kwake ni Paroko wa Parokia ya Kitunda na Mganga Mkuu wa Wilaya. Kushoto kwake ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea Mhashamu Nobert Mtega, akifuatiwa na Mbunge wa jimbo la Ukonga Eugene  Mwaiposa na Mama Mkuu wa Shirika Sista Maria Shukrani Mkonde.
Watumishi wa Kituo cha Afya cha Mt. Benedikt kilichopo Kitunda wakiwa kwenye picha ya pamoja mbele ya chumba cha wagonjwa nje baada kuzinduliwa rasmi kwa  Kituo hicho na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik  akihutubia hadhara ya wakazi wa Kitunda waliohudhuria kwenye shamrashamra za kuzindua Kituo cha Afya cha Mt. Benedikt katika Kata ya Kitunda manispaa ya Ilala. Kulia kwake ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea Mhashamu Nobert Mtega na kulia ni Mama Mkuu wa Shirika la Masista la Wabenedikt la Mt. Agnes  ambalo ndilo linamiliki kituo hicho kwa asilimia 100.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik akikata keki iliyoandaliwa rasmi kwa ajili ya shamrashamra za uzinduzi wa Kituo cha Afya cha Mt. Benedikt katika Kata ya Kitunda.PICHA ZOTE/DAILY MITIKASI BLOG

No comments: