Tangazo

October 25, 2011

UBALOZI WA UTURUKI WATOA MSAADA WA INCUBATORS 10 KWA TAASISI YA WANAWAKE NA MAENDELEO (WAMA)

Balozi wa Uturuki  nchini Tanzania, Dkt. Sander Gurbuz akitoa maelezo kwa  Mwenyekiti wa Taasisi ya  WAMA, Mama Salma Kikwete  namna ya kutumia incubator wakati wa makabidhiano ya incubators 10 kwa ajili ya watoto wachanga yaliyofanyika katika ofisi za Taasisi ya WAMA, Oktoba 24, 2011.
Balozi wa Uturuki  nchini Tanzania' Dkt. Sander Gurbuz  akikabidhi incubators 10  zenye thamani ya Tsh. Millioni 50/- kwa ajili ya kusaidia kuboresha huduma kwa watoto wachanga kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete. Wanaoshuhudia ni Mke wa Balozi wa Uturuki nchini , Mama Durhan Gurbuz na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la TPM Mining and Energy Co. Limited, Bw. Burak Buyuksarac - Oktoba 24, 2011.
Picha ya pamoja  baada ya makabidhiano ya incubators 10 zenye thamani ya Tsh. Millioni 50/- kwa Taasisi ya WAMA yaliyofanyika katika ofisi za WAMA, Oktoba 24, 2011.
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA ,  Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mke wa Balozi wa Uturuki, Mama Durhan Gurbuz wakati wa makabidhiano ya incubators 10 yaliyofanywa na Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania, katika Ofisi za WAMA, Oktoba 24, 2011.
Balozi wa Uturuki  nchini Tanzania, Dkt. Sander Gurbuz akimweleza Mama Salma Kikwete, Mwenyekiti wa WAMA  kuhusu msaada wanautoa wa incubators 10 kwa Taasisi ya WAMA. Kulia kwa balozi ni Mke wake  Mama Durhan Gurbuz na  (kushoto) kwake  ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la TPM Mining and Energy Co. Limited, Bw. Burak Buyuksarac - Oktoba 24, 2011.
                                    *********************************************
 Habari & Picha/WAMA Foundation
Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania umetoa msaada wa incubators 10 zenye thamani ya Tsh. Mil 50/- kwa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inayoongozwa na Mhe. Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Akikabidhi msaada huo Balozi wa Uturuki hapa nchini Mhe. Dr. Sander Gurbuz amesema kuwa wametoa msaada huo kwa ajili ya kusaidia moja ya programu za Taasisi ya WAMA inayolenga kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto.  Pamoja na kudumisha uhusiano mzuri ambao nchi yake ya Uturuki na Tanzania umekuwa nao. Mhe. Balozi aliambatana na Mke Wake Mama Durhan Gurbuz na Mkurugenzi Mkuu wa TPM Mining and Energy Co. Limited, Bw. Burak Buyuksarac.

Akitoa shukrani baada ya kupokea  msaada huo Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mhe. Mama Salma Kikwete amesema kuwa msaada huo ni mkubwa sana  na utasaidia kuokoa maisha ya watoto wachanga ambao wangeweza kufa kutokana na ukosefu wa vifaa hivi hasa maeneo ya vijijini. Mama Salma aliongeza kuwa pamoja  mazingira ya Vijijini yanaweza yasiruhusu sana utumiaji wa vifaa hivi lakini kwa sababu siku hizi kuna umeme wa jua  utasaidia matumizi ya vifaa hivi.

No comments: