Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Ananilea Nkya |
Wahariri wapatao 50 kesho Jumatano Oktoba 05, watakutana jijini Dar es Salaam kujadili jinsi vyombo vya habari vinaweza kutoa mchango mkubwa zaidi kuchangia juhudi za taifa za kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake, wasichana na watoto.
Wahariri hao wanatarajiwa kuanngalia ni mambo gani ambayo wao wenyewe na vyombo vyao vitaweza kufanya ili viongozi na wananchi mijini na vijijini wachukue hatua kuepusha vitendo vya ukatili wa kijinsia visitokee katika maeneo yao.
Kadhalika watajadili ni mikakati gani vyombo vya habari vinaweza kuweka ili kuweza kuibua matukio ya vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake, wasichana na watoto ili huduma stahili za kimatibabu, kisheria na ushauri ziweze kutolewa kwa waathika wa vitendo hivyo viovu.
Chama Cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya idadi ya watu (UNFPA) wameandaa mkutano huo wa wahariri ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya kitaifa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa sababu vitendo hivyo vinarudisha nyuma maendeleo ya familia na taifa.
Wahariri hao watakaokutana katika ofisi za TAMWA, Sinza Mori kuanzia saa 4.30 asubuhi hadi saa saba mchana watapata fursa pia ya kupata taarifa kuhusu hali halisi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia hapa nchini na jitihada kadhaa zinazochukuliwa kukabili tatizo hilo.fisi
Vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake, wasichana na watoto ni pamoja na vipigo, ubakaji, ukeketaji, kudhulumu wajane hazi za mirathi, ndoa na mimba za utotoni na kutelekeza watoto kunakoongeza watoto kuishi mitaani.
Tunaamini kuwa vyombo vya habari vikitumika ipasavyo kufanya tatafiti, kutangaza na kufuatilia hatua kwa hatua kesi za matukio ya ukatili dhidi ya makundi haya wadau watachukua hatua stahiki kupunguza tatizo hilo.
Wadau wanapaswa kufanya juhudi kubwa kuepusha ukatili wa kijinsia ni pamoja na viongozi wa umma wakiwepo wa vitongoji, vijiji na mitaa, madiwani, wabunge, polisi, mahakama, mashirika ya kijamii, madhehebu ya dini, wizara mbali mbali, wafadhili, waathirika na umma kwa ujumla wanawake na wanaume mijini na vijijini.
Tafiti zinaonesha kuwa ukatili wa kijinsia ni matokeo ya kutokuwepo haki sawa katika jamii baina ya wanaume na wanawake na kwamba vitendo hivi vina madhara makubwa kwa afya na ustawi wa wanawake.

Imetolewa na:
Ananilea Nkya
Mkurugenzi Mtendaji
Ananilea Nkya
Mkurugenzi Mtendaji
No comments:
Post a Comment