Tangazo

October 24, 2011

Wizara ya Mawasiliano na Airtel watembelea Tanga kutathmini jinsi ya kuboresha mawasiliano vijijini

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,  Charles Kitwanga (kushoto) akimsikiliza Afisa Masoko wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Marecha Edward (kulia) wakati alipotembelea moja ya minara ya mawasiliano ya Airtel uliopo Muheza, Mkoani Tanga mwishoni mwa wiki ikiwa ni sehemu ya Ziara yake katika Mkoa wa Tanga. Katikati ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini,   Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu" akionyesha simu yake kwa Afisa Masoko wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Marecha Edward wakati kampuni hiyo ilipotembelea kijiji  cha Bombo Maji Moto, Kata ya Kizari wilaya ya Korogwe Vijiini ili kuona hali ya mawasiliano ilivyo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,  Charles Kitwanga (wa pili kulia) pamoja na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini,  Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu" (kulia) wakimsikiliza mmoja wa wananchi wa kijiji cha Kijango Magoma aliejitambulisha kwa jina la Mzee Khalifa (mwenye kofia) alipokuwa akielezea hali ya mawasiliano katika kijiji hicho wakati wa ziara maalum ya Naibu Waziri ya kuangalia hali ya mawasiliano wilayani humo. Kushoto ni Afisa Masoko wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Marecha Edward.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,  Chiku Gallawa (kulia) akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,  Charles Kitwanga (katikati) ambaye aliambatana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya walipokuwa wakitathmini hali ya Mawasiliano ya simu za mkonini na jinsi ya kuyaboresha katika mkoa huo wa Tangamwishoni mwa wiki.

No comments: