Tangazo

November 11, 2011

Bondia Rashid Matumla kudundana na Maneno Osward Desemba 25 jijini Dar

Rashid Matumla 'Snake Boy"
Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ wanatarajia kupanda ulingoni  kuzichapa Desemba 25  mwaka huu katika pambano lisilo la ubingwa.

Pambano hilo linatarajia kuwa  la raundi 10 uzito wa kati  litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam .

Akizungumza Dar es Salaam jana  Ofisa habari wa Kampuni Adios Promotion ambao ndio waandaaji wa pambano hilo, Mao Lofombo alisema  pambano hilo limeandaaliwa ili kumaliza ubishi baina ya mabondia hao ambapo katika pambano la mwisho Matumla alimchapa Oswald kwa pointi ambaye aliwalalamikia majaji kuwa hawakumtendea haki wakati walishawai kupigana mara mbili nyuma ambapo Matumla kamshinda Maneno Mara mbili na Maneno kashinda mara moja mpambano huo utakuwa wa kumaliza ubishi baina yao.

Alisema tayari mabondia hao wamekubali kucheza pambano hilo ambalo litakuwa la marudiano na kwamba  wameshaanza maandalizi  ambapo kila mmoja amejigamba kumstaafisha mwenzie ngumi.

Mao alisema, licha ya pambano hilo linalotarajia kuvuta hisia za mashabiki wa ngumi, pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambapo Rashidi Ally atachapana makonde na Hassan Sweet, Kalulu Bakari na  Athuman Kalekwa na  Shabani Kazinga na Kashinde'

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

No comments: