|
Kijana Emi, akionesha umahiri wake katika mchezo wa sarakasi kama alivyonaswa na kamera yetu nje ya Leecars Pub eneo la Namanga jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. |
|
Pamoja na udogo wangu naweza kummudu huyu Brooo... |
|
Naweza kukaa juu ya ncha za misumari kuna mtu anabisha....??? |
|
Dogo anaonesha uwezo wake.... |
|
Kaka mtu anasema na yeye pia ana makalio ya chuma kwani misumari haiwezi penya na kumdhuru.. |
|
Vile vile naweza hata kusimamia uso kwenye ncha za misumari....duuuuuu hii hatari.. | | | | | | | | | | | |
|
|
Mapema wiki hii kamera ya Daily Mitikasi Blogu iliweza kuwanasa vijana hawa ambao huyaendesha maisha yao kupitia vipaji walivyopewa na mwenyezi Mungu wakionesha shoo ya kufa mtu nje ya Leecars Pub iliyopo eneo la Namanga- Msasani jijini Dar Es Salaam ambapo hucheza sarakasi katika maeneo mbalimbali ya Jiji hilo na ujira wanaoupata huwawezesha kuishi.
Vijana hao waliojitambulisha kwa majina ya Emi na mwingine mdogo Alphonce Ronald Maro (9) anaepiga kitabu Darasa la Pili katika Shule ya Msingi Jangwani Beach wamesema kwa siku hujipatia kiasi cha 5,000/- kutokana na kazi hiyo ya kuburudisha watu lakini mambo yakiwa safi hupata hadi 10,000/-. PICHA/Daily Mitikasi Blogu
No comments:
Post a Comment