Tangazo

November 10, 2011

NHIF NA TUZO YA HUDUMA BORA NA USHIRIKI ULIOTUKUKA KWENYE MAONESHO YA MIAKA 50 NA HIFADHI YA JAMII KWA WOTE

MKURUGENZI WA OPERESHENI WA NHIF, BW. EUGEN MINGONGOTI AKIPOKEA TUZO YA USHIRIKI ULIOTUKUKA  KATIKA KUTOA HUDUMA BORA ZA AFYA KWA NIABA YA MKURUGENZI MKUU, KUTOKA KWA WAZIRI WA KAZI AJIRA NA MAENDELEO YA VIJANA MHE. GAUDENSIA KABAKA WAKATI WA UFUNGUZI WA MAONESHO YA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII INAYORATIBIWA NA MAMLAKA YA HIFADHI YA JAMII (SSRA)YANAYOENDELEA  KWENYE VIWANJA VYA MNAZI MMOJA.

WAKIFURAHIA KWA PAMOJA TUZO HIYO KWENYE BANDA LA NHIF AMBAPO MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA UMEIPATA KUTOKANA UTOAJI WA HUDUMA ZA UPIMAJI WA AFYA BURE KWA WANANCHI NA WANACHAMA WAKE ,ANAYEFURAHIA KATI  NI MKURUGENZI WA OPERESHENI BWN.E.MINGONGOTI,KUSHOTO NI MKURUGENZI WA FEDHA BWN. DEUSDEDIT RUTAZAA KULIA NI OFISA WA IDARA YA UANACHAMA BI. NEEMA MSANYA.

UPIMAJI WA KISUKARI UNAFANYIKA BURE KWA WANANCHI NA WANACHAMA WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA PICHANI NI DKT. ESHE JUMA WA NHIF AKIMPIMA BWN. MOHAMED JUAKALI SUKARI KWENYE BANDA LA MFUKO.KARIBUNI WOTE KWANI HUDUMA NI BURE.

No comments: